Umekazana kuwaambia marafiki zako 'Siku hizi hakuna Mapenzi ya dhati watu wote Majanga tu', nani amekwambia hayapo?? Yapo sana ila wewe unatumia mbinu tofauti. Hauwezi kusoma Degree ya Law harafu ukatuma maombi ya kazi ya Chief Accountant wa Bodi ya Tumbaku hapo utakuwa kila siku unasingizia Balance Sheet haina Jurisprudence... Lawyers mmenielewa!

Acha kudate watu wasiojielewa, Usidate na mtu kwa sababu uko lonely, Usiwe desperate kuingia Mahusiano kwa sababu shosti zako wanakusimulia walivyopelekwa Rwenzori Waterfalls, Marangu Waterfalls, Mbuga za Saadan, Maisha Club n.k... Ingia kwenye Mahusiano pale Moyo wako ukiwa tayari na mtu uliyemfia kihisia na amekuwa approved na Veins, Auricles, na Aorta za Moyo wako kwamba He/She is really the One.

Unadate na mtu ambaye mustakabali wake mwenyewe haujui, ukimuuliza anataka kuwa wapi ndani ya miaka 5 ijayo anakwambia Mungu anajua don't worry, halafu BBM na Instagram unajiita 'Baby Ake Mie Iam in Love'.. Utaishia kufua boxer hadi kucha zinukie gololi!

Mbwa kamwe hashughuliki na kesi za Paka kufungiwa kabatini. Date the Right Person, With Right reasons, in a Right Time uone kama Mapenzi hayapo. Jipange mapenzi ya kweli yapo na yamejaa tele. Nimemaliza!

Imetolewa na 
Mkuu wa Chuo cha Mapenzi
Seth Giovanni
Majira ya saa 2 usiku ameokotwa mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na miezi mitatu karibu na kiwanda cha Bidco karibu na magorofa ya bima kando ya dimbwi la maji huku mtoto huyo akiwa hajavalishwa nguo.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliofika eneo la tukio na kumchukua mtoto huyo na kumpeka kituo cha polisi Mikocheni 'B', jijini Dar es Salaam walisema kuwa walishangaa kusikia kilio cha mtoto mchanga ndipo waliposogea eneo la tukio na kukuta mtoto huyo akiwa eneo la tukio akiwa peke yake katupwa bila nguo.

Mashuhuda hao wamesikitishwa na kitendo hicho na kuomba jamii kuacha matendo ya unyanyasaji ambayo imekuwa ikiyafanya.
Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo. Wengine pichani kutoka kushoto ni DJ John Dilinga (JD), Prodyuza Ally Baucha na Prodyuza Tudd Thomas.
Kutoka kushoto waliokaa ni msanii Stamina, DJ John Dilinga, Abdallah Mrisho, Ally Baucha na Tudd Thomas katika picha ya pamoja na washiriki wa The Vodacom Mic King waliosimama nyuma.
Wakali wa MIC wanaowania gari wakiwa katika pozi na gari hilo.
Wanahabari wakichukua baadhi ya matukio.
...Wakimsikiliza Abdallah Mrisho.

Hawa ndiyo wakali tisa wanaowania gari aina ya Toyota Funcargo (New Model).
Uongozi wa Dar Live Co. Ltd leo umetambulisha tamasha kubwa la kila mwaka la Usiku wa Hip Hop na fainali za kumtafuta Mkali wa Mic zijulikano kama 'The Vodacom Mic King' kwa wanahabari. Tamasha hili litafanyika Jumamosi hii, Mei 25, 2013 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar. 

Jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi ataondoka na gari aina ya Toyota Funcargo (New Model) yenye thamani ya shilingi milioni 15. Mbali na zawadi ya gari, mshindi wa kwanza, pili na watatu, watapata fursa ya kurekodi wimbo mmoja chini ya Prodyuza mahiri nchini, Tudd Thomas, aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka Dutigite wa Kigoma All Stars na nyingine nyingi. Majaji katika shindano hili ni mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho, DJ John Dilinga (JD) na Prodyuza Ally Baucha.
Tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa wakali wa Hip Hop nchini ambao ni Fid Q, Joh Makini, Stamina, Kala Jeremiah, Nay wa Mitego pamoja na shoo kali kutoka kundi la Wakali Dancers. Katika usiku huo, zitatolewa tuzo kwa wasanii wa Hip Hop na kwa wimbo bora wa Hip Hop uliofanya vizuri mwaka 2012/13. Kutakuwa na Tuzo kwa Msanii Mkongwe Bora wa Hip Hop na Msanii Chipukizi Bora wa Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop.
(PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)
Baada rais Barack Obama kutangaza kutembelea nchi 3 barani Afrika, bila kutembelea nchi yake ya asili ya Kenya, sasa Wakenya wahoji na kuona kuwa rais huyo ni msaliti.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog, wakenya hao walisema kuwa wanasikitishwa na kitendo cha rais huyo kuitembelea nchi ya Tanzania na kuiacha nchi yao ya Kenya.

"Tunasikitishwa sana na rais huyu wa Marekani Barack Obama kutembelea nchi ya Tanzania na kuiacha nchi yetu, maana wakenya wanahamu nae tokea ameingia madarakani ila amekuwa kimya hata kuja kuwasalimia licha ya kumtumia salamu za pongezi rais wetu Uhuru Kenyatta," Walilalama Wakenya hao.

Kuanzia tarehe 26 Juni hadi 3 Julai, Rais Obama na Mkewe wanatarajia kutembelea nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania. Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.

Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa. Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii na duniani kote kwa ujumla.
John Gatt-Rutter, the European Union Representative in Jerusalem, Monday confirmed that the EU is still considering labelling the products of the illegal Israeli settlements in Palestine.

He denied, during a lecture held in the Arab American University in Jenin about EU’s position regarding the Palestinian-Israeli conflict, what has been circulating through media about EU’s intention to postpone labelling the illegal products over US intervention.

Gatt-Rutter affirmed that EU and Palestine have deep-rooted relations based on international legitimacy and recognition of the Palestinian right to self-determination and right to establish an independent state within 1967 borders with East Jerusalem as its capital.

He said that labelling these products will make it known to the European consumer that these are the products of illegal settlements in Palestine.

Gatt-Rutter further added that these products will not be given the privileges given to the Israeli products in the European market.

EU’s position regarding settlement activity remains clear and solid; it is illegal, and undermines peace efforts while jeopardizing in the process the dream of a Palestinian state, he said.

Gatt-Rutter also called on Palestinians to hold democratic elections to address the world and gather international support at the international forums.

He also affirmed that the prisoners’ cause receives immense attention by the EU through monitoring their humanitarian and health status and ensuring their rights as prisoners
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Professa Jay ametangaza rasmi kuwa mwanachana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria bunge la bajeti jana. Kwa mujibu wa picha ambazo amekuwa akizisambaza kwenye mitandao ya kijamii msanii huyo alionekana akiwa na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi huku akiwa amekamatia kadi ya chama hicho.

 Mtoto aliyezaliwa jana George Kivaria Akiwa amepigwa na butwaa baada ya kupewa suprisezzzzz na baadhi ya wafanyakazi wa idara yake wakati alipokumbushwa siku yake ya kuzaliwa hapo jana
 Mh George Kivaria akiwa na furaha wakati wafanyakazi wa idara yake walipomuandalia zawadi ndogo ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake hapo jana japokuwa alikataa kututajia umri wake.
 Suprizeeeeeeee Mtoto aliyezaliwa jana Mh George Kivaria (Wa kwanza Kushoto) akipiga picha keki aliyoletewa na wafanyakazi wa idara yake hapo jana.
 Mtoto aliyezaliwa jana Mr George Kivaria Mkuu wa Idara ya Njia Mbadala aka Alternative Channel ya NMB akikata keki tayari kwa kuwalisha wafanyakazi wa idara yake.
 Kata Keki tule.........ndio muda huo uliwadia
 Keki ilipoanza kuliwa.
 Uzaliwe tena ndio maneno yaliyosikika hapo.....
 Keki tamu hadi inataka kudondoka. Happy Birthday Mr George baada ya Kulishjwa  Keki
 Operation meneja wa Njia Mbadala Mr Kilongo naye akipatiwa kipande Cha Keki

Happy Birthday Mr George Kivaria Mungu Akuzidishie Nguvu, Upendo na Heri ya Miaka Mingi hapa Dunia.
Prodyuza Tudd Thomas.

MASHABIKI wa mtayarishaji wa muziki (Producer), mwenye uwezo wa kipekee, aliyetayarisha wimbo wa Leka dutigite wa Kigoma All Stars na zingine nyingi, Tudd Thomas, wamekuwa wakiulizana maswali mengi wao kwa wao pasipo kupata majibu.

Safari ya Tudd Thomas katika muziki, ilianzia mkoani Iringa akiwa Iringa Records aliporekodi wimbo wa mwanamuziki Marlaw unaoitwa Bembeleza. Wimbo huo ulipata tuzo ya wimbo bora wa mwaka kutoka Kilimanjaro Tanzania Music Awards mwaka 2008 na pia kumfanya Marlaw apate tuzo ya msanii bora wa kiume kupitia tuzo hizo. Baadae alihamia jijini Dar es Salaam na ndipo alipoonesha uwezo wake zaidi kwa kusuka nyimbo zilizotikisa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Hakuna asiyeufahamu wimbo wa Pii Pii (Missing my baby) wa Marlaw ambao aliutengeneza yeye kupitia Studio ya JML. Wimbo huo ulipata tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na tuzo ya Nzumari nchini Kenya mwaka 2009 mbapo uliingia kwenye kipengere cha wimbo bora wa Afrika Mashariki, kumfanya Marlaw aingie kwenye kipengele cha msanii bora wa Afrika Mashariki na kunyakua tuzo hiyo. Baada ya hapo wimbo huo ulipata tuzo ya Kilimanjaro nchini Tanzania kama wimbo bora wa mwaka wa Afro pop mwaka 2010, tuzo ya Chaguo la Teneez Music nchini Kenya kama wimbo ulioongoza kwa kuchukuliwa kwa njia ya mtandao Afrika Mashariki “The most downloaded East African song” mwaka 2010, pamoja na tuzo ya Nigeria Sound City Video Music kama wimbo bora wa Afrika Mashariki mwaka 2010.

Aliendelea kutayarisha nyimbo ambazo zilipata umaarufu mkubwa na kuingia kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo za muziki za Kilimanjaro. Mwaka 2012, nyimbo tatu zilizotokana na mikono yake zilipata nafasi ya kushiriki tuzo hizo. Nyimbo hizo ni Liz One wa Izzo Business ambao uliingia kwenye vipengele viwili ambavyo ni wimbo bora wa mwaka na wimbo bora wa Hip hop na pia kusababisha msanii huyo aingie kwenye kipengele cha msanii bora wa Hip hop. Milele daima wa Barnaba na Kizunguzungu wa Rachel, ambapo zote ziliingia kipengele cha wimbo bora wa Zouk/Rhumba pia ni nyimbo alizotengeneza mtayarishaji huyo.

Nyimbo zingine alizotayarisha ambazo zilifanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV ni Kisa pombe na Soldier za Mwasiti, Sorry sana, Mbayuwayu na Mtoto wa Afrika za Marlaw pamoja na Natumaini ya Becka aliyowashirikisha Barnaba na Amin. Pia zipo nyingine kama Unikimbie ya Amin, Tushukuru kwa yote ya Ditto, Lonely ya Linah na Magubegube ya Barnaba.

Mtayarishaji huyo ambaye hajawai kuingia kwenye tuzo za Kilimanjaro za muziki wa hapa nchini Tanzania ambazo mwaka huu zimeongezewa kipengele cha Mtayarishaji bora chipukizi ndiye aliyetayarisha wimbo wa Leka dutigite wa Kigoma All Stars kupitia Studio yake ya Ngoma Records. Wimbo huu umeingia kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka 2013. Pia alishirikiana na mtayarishaji Imma the boy kutengeneza wimbo wa Me ‘n’ U wa Ommy Dimpoz ambao umeingia kwenye kipengele hicho na vipengele vingine ambavyo ni wimbo bora wa Bongo Pop na wimbo bora wa kushirikiana.

Alipoulizwa alisema hapendi kuzungumzia juu ya kutotajwa kama miongoni mwa wanaowania tuzo. Aliendelea kusema kwamba, hata kama baadae ikitokea, kwake ni motisha tu, lakini kikubwa zaidi ni kwamba anahisi analo deni kubwa la kutumia uwezo wake ipasavyo kufanya kazi nzuri zaidi ya hapo ili kuutangaza muziki wa Tanzania kimataifa. Pia alisema ana malengo makubwa aliyojiwekea na ndiyo maana kila kukicha anawaza kutayarisha nyimbo zenye tofauti na zenye radha ya kipekee.

Tudd Thomas anaendelea kukitumia kipaji chake na ujuzi wake ipasavyo na siku chache zilizopita kuna nyimbo zisizopungua tatu zilizoingia sokoni na zinafanya vizuri, ambazo ni kazi za mikono yake. Nyimbo hizo ni Uswazi take away ya Chegge, Nyumbani ya Kigoma All Stars na pia ameshirikiana kwa kiasi kikubwa na mtayarishaji Fundi Samwel kutengeneza wimbo wa Mahakama ya mapenzi wa Linex.
Ilikuwa ni simanzi, vilio na pigo kwa familia nyingi.
 Kumbukumbu zinaonyesha Meli hiyo ilikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote. Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo. Ambapo meli ilizaman umbali wa kilomita 30 kukaribia kutia nanga bandari ya Mwanza.

RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37.

Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.

Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema haina dini, huongozana na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga, kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.

Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa mv Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru, (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa; aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.

Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001. Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi, ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Hukumu ya kesi ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay (sasa mstaafu), Ijumaa, 29 Novemba 2002, majira ya saa sita mchana.

Washitakiwa wote walishinda kesi, kufuatia hukumu ya kurasa 118 iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay kusema, mv Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano wa majini na siyo uzembe wa washitakiwa.

Serikali iliahidi kukata rufaa; lakini hadi leo majaliwa ya rufaa hiyo hayajulikani; na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia bila kujua hatma ya kesi hiyo wala stahili zao.

Kwa kipindi kirefu, mv Bukoba ilikuwa ‘kaburi’ lenye kuelea katika Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa marufuku kufanya safari kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora wa kuwa majini.

Meli hii ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji; ikazinduliwa 27 Julai 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti na ilikosa uwiano.
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwakamata askari 16 wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya magendo, askari wengine wawili wa jeshi hilo wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa na shehena kubwa ya bangi wakiisafrisha kwenda nchini Kenya.

Askari hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu saa nne usiku eneo la Kilemapofu, Wilaya ya Moshi Vijijini wakiwa na magunia 18 ya bangi ambayo walikuwa wameyapakia kwenye gari la Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2025.

Akithibitisha kukamatwa kwa askari hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz (PICHANI) alisema askari hao walikuwa wakipeleka bangi hiyo Wilaya ya Rombo kwa mfanyabiashra mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake.

Kamanda Boaz aliwataja askari waliokamatwa na wanashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi katika mji mdogo wa Himo kuwa ni F.1734 Koplo Edward (dereva) wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Arusha na G.2434 Konstebo George wa kituo cha polisi Ngarenanyuki Wilaya ya Arumeru.

Alibainisha kuwa kukamatwa kwa askari hao kunatokana na operesheni ya kukabiliana na dawa za kulevya inayofanywa na polisi katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Alisema operesheni hiyo imefanyika kikamilifu katika Mkoa wa Arusha uliokuwa ukitumika kupitishia bidhaa hiyo, na sasa wahusika wameamua kuutumia Mkoa wa Kilimanjaro.

“Baada ya kuwahoji askari wale, walidai kuwa walikodishwa na mfanyabiashara huyo kuipeleka bangi hiyo wilayani Rombo tayari kwa kusafirishwa kwenda nchini Kenya ambako inaaminika kuna soko kubwa,” alisema.

Kamanda Boaz alisema hivi sasa polisi wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha wanafanya uchunguzi kubaini mtandao wa askari hao unaojihusisha na vitendo haramu.

Aliongeza kuwa hatua inayofuata kwa askari hao ni kufunguliwa mashtaka ya kijeshi na iwapo watakutwa na hatia watafukuzwa kazi kisha watafikishwa katika mahakama za kiraia.

Kamanda Boaz alibainisha kuwa kwa kawaida askari wanapotoka mkoa mmoja kwenda mwingine hupatiwa kibali maalumu cha kusafiria (Movement Order). Alisema kibali hicho husaini kila mkoa ambao askari husika hupita, lakini waliokamatwa na bangi hawakuwa nacho.

Kamanda Boaz alibanisha kuwa kwa hali ilivyo askari hao waliondoka na gari la mkuu wa FFU bila kumpa taarifa wala kupata kibali chake.
Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obsessed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!

Kuna Ndoa na kuna Harusi... Wengi mnapenda zaidi harusi,na mnapowaza Ndoa picha inayowajia ni Suti kali,Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Alingo, Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall..

Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi??

Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi. Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako???

Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize, Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi???? Alamsiki...Wa kukopi mnakaribishwa ila vigezo na masharti kuzingatiwa!

Imetolewa na 
Mkuu wa Chuo cha Mapenzi
Seth Giovanni

MSHINDI WA TAJI LA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 HADIJA SAID MISS UTALII MOROGORO  KATIKATI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM KUSHOTO NA MSHINDI WA TATU KULIA THELESIA KILOMO MISS UTALII VYUO VIKUU.
 MSHINDI WA TAJI LA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 HADIJA SAID MISS UTALII MOROGORO AKISHWA TAJI LA USHINDI NA MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI KANALI MSTAAFU CHIKU GALAWA,MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA BENDEGO.
KUTOKA KUSHOTO NI MISS UTALII KUTOKA MKOA WA KATAVI ASHA RAMADHANI ALIYE SHINDA NAFASI YA NNE, LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM ALIYESHINDA NAFASI YA PILI, MISS UTALII MOROGORO HADIJA SAID AMBAYE NDIYE MISS UTALII TANZANIA 2012/13, MISS UTALII VYUO VIKUU THERESIA KILOMO.

 KUTOKA KUSHOTO NI MISS UTALII KUTOKA MKOA WA KATAVI ASHA RAMADHANI ALIYE SHINDA NAFASI YA NNE, LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM ALIYESHINDA NAFASI YA PILI, MISS UTALII MOROGORO HADIJA SAID AMBAYE NDIYE MISS UTALII TANZANIA 2012/13, MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI KANALI MSTAAFU CHIKU GALAWA,MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA BENDEGO ,MISS UTALII VYUO VIKUU THERESIA KILOMO NA MISS UTALII SINGIDA MWAKOMBO KESSY ALIYESHINDA NAFASI YA TANO.

 WASHIDI WA TANO BORA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI MKOA WA TANGA.
PLO official Hanan Ashrawi on Sunday condemned the European Union's decision to delay the labeling of settlement products following a request from US Secretary of State John Kerry.

"This once again brings into question the American role in negotiations as a credible mediator," Ashrawi said in a statement.

"Rather than providing Israel with immunity, the Obama administration should act responsibly and promote prospects for a just peace and Palestinian self-determination and freedom."

The senior PLO official said the EU should go further than simply labeling settlement products by enforcing a "serious ban" on their sale.

"The US has used the so-called peace process as an instrument of Israeli impunity; it is about time to end such a policy."

EU foreign ministers from 27 member states agreed over a year ago to enforce EU legislation and label products originating from illegal settlements in the occupied West Bank.

On February 22, EU foreign policy chief Catherine Ashton called on EU foreign ministers to enforce legislation on labeling settlement goods and in April, 13 EU foreign ministers expressed support for the initiative, with the issue currently in discussion.

US Secretary of State John Kerry and senior US officials reportedly asked Ashton to delay enforcement of the proposal, with the Americans saying that it would harm Kerry's efforts to restart peace talks.

A senior Israeli official told the Israeli daily that Israel had asked the US administration to intervene to delay the EU's decision to follow through on labeling settlement products.

The decision to label settlement goods will likely be delayed until June.
Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la mkutafuta malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu "Redd's Miss Tanga 2013" litafanyika Juni 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani,Mkoani humo.

Akizungumza na gazeti hili jana Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, alisema kuwa warembo tayari wameanza mazoezi yakatofanyika kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.

Kigundula alisema shindano hilo litaanza saa 2, usiku, ikiwa ni pamoja na kuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa moja ya bendi maarufu hapa nchini pamoja na wasanii wanaotamba katika muziki wa kizazi kipya.

Alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri jumla ya warembo 14 watashindania taji hilo.

Kigundula alisema kuwa mpaka juzi warembo 10 wamejitokeza na kuanza mazoezi yanayosimamiwa Miss Tanga 2012 Teresia Kimolo na Mwanaid Omar.

Hawa Ramadhan (18), Hazina Mbaga (19), Like Abdulraman (19), Jack Emannuel (18), Waida Mmbwambo(20), Tatu Hussein(19), Mwanahamis Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21), Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21).

"Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake"alisema Kigundula

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

Redd's, Miss Tanga, imedhaminiwa na CXC Africa, Executive Solutions, Busta General Supply, Mkwabi Interprises, Lusindic Investment LTD, Lavida Pub, Jambo Leo, Staa Spoti, Five Brothers, Clouds Media Group, pamoja na Michuzi Media Group, Bongostaz.com, Saluti5, Kajunason Blog, JaneJohn, na Kidevu blog.