Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba kutoka Morogoro (wa kwanza kushoto) akiwa na uso wa furaha na binti yake Irene Hatibu (wa pili kushoto) muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake. Wa kwanza kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa. Wengine ni Viongozi wa Tigo Kanda ya Pwani.
Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba kutoka Morogoro akijifuta machozi ya furaha muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kulia ni mtangazaji wa Radio Clouds FM Mina Ally na wengine ni viongozi wa Tigo kanda ya Pwani.
Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba kutoka Morogoro (wa tatu kulia), akiwa na washindi wa shilingi milioni moja moja kutoka mkoani Morogoro muda mfupi baada ya wote kukabidhiwa zawadi zao. Kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally na wengine ni viongozi wa Tigo Kanda ya Pwani
Mmoja wa washindi wa zawadi ya shilingi milioni moja wa Promotion ya Tigo Jigiftishe Suleimani Ndago (wa kwanza kushoto) kutoka Morogoro akicheza muziki muda mfupi kabla kukabidhiwa zawadi yake mjini Morogoro. Wa kwanza kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally na anayefuatia ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa
Na Mwandishi Wetu.
Zawadi ya wiki ya shilingi milioni kumi inayotolewa katika kampeni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe, ilikabidhiwa mwishoni mwa wiki kwa Flora Somba ambaye ni mkazi mjini Morogoro .
Flora anakuwa ni mshindi wa nne kupata zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga wote wa Dar es Salaama pamoja na Mbwana Mbela mkazi wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Akiongea huku akibubujikwa na machozi wakati akikabidhiwa zawadi yake, Flora ambaye anafanya kazi za vibarua kwenye ujenzi kama kubeba zege, alisema Mungu amemtendea miujiza kupitia Tigo Jigiftishe.
“Nalea watoto wawili peke yangu, mimi ndiyo baba na mimi ndiyo mama. Binti yangu Irene alilazimika kuacha shule kwa sababu sikiuweza kumlipia ada, nashukuru Mungu sasa ataweza kurudi shuleni,asante Tigo kwa kubadilisha naisha yangu” alisema
Flora alisema fedha atakazopata pamoja na kusaidia ada za watoto, atajitahidi kujenga nyumba walau ya vyumba viwili ili kuachana na nyumba za kupanga na kuongeza kuwa fedha itakayobaki atafungua biashara itakayomsaidia kuhudumia familia yake.
Hafla ya kukabidhi mshindi wa milioni 10 zawadi yake, ilienda sambamba na kuwakabidhi washindi wengine saba wa shilling milioni moja moja kutoka mkoa wa Morogoro zawadi zao
Akiongea wakaati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Tigo kwa Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema promosheni ya Jigiftishe inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu.
“Leo mmeshuhudia tukimkabidhi mshindi wa milioni 10 zawadi yake pamoja na washindi wengine saba ambao kila mmoja amepata shilingi milioni moja kutoka hapa Morogoro. Kila mtu ambaye anatumia mtandao wa Tigo anaweza kushinda endapo ataendelea kutumia huduma za Tigo kama kuweka muda wa maongezi, kutuma Pesa, kununua umeme na huduma nyingine,” alisema
Mutalemwa alisema alisema zawadi za milioni 10 na milioni moja bado zipo na kuongeza kuwa mshindi mkubwa atajinyakulia shilingi milioni 50 huku wengine wawili wakijinyakulia shilingi milioni 25 na 15.
Toa Maoni Yako:
0 comments: