Meneja Mradi, Ushirikishwaji wa Vijana - TYVA, Alfred Kiwuyo akiwaelezea washiriki dhima ya kongamano la vijana waliokutana kujadili haki na wajabu kwa vijana katika maendeleo ya Taifa. (Picha na Geofrey Adroph)

TYVA ni asasi ya vijana ambayo imejikita na Kujipambanua kupigania jamii yenye haki na usawa, amani na misingi ya kidemokrasia na yenye ushiriki hai na wenye tija kwa vijana katika shughuli za maendeleo imeandaa kongamano hili kuwawezesha vijana kujadili Haki na Wajibu kwa Vijana na mstakabali wa Taifa kwa ujumla. Kongamano hili pia lilikuwa na dhima ya kupanua uelewa na umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendele ya Taifa kwa ujumla.
Wakili Chikulupi Kasaka, akitoa mada ya Haki na Wajibu wa Vijana kwa vijana mbalimbali wa vyoni na mtaani waliokuta kujadili haki na wajibu wao katika jamii iliyofanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es salaam iliyoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA .
Mwenyekiti wa Bodi ya washauri ya Vijana (YAB) Femina Hip, Hassan Pukey akitoa mada kwa vijana waliofika katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA ili kujadili haki na wajibu wa vijana na katika jamii.
Makamu Mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumzia mchakato wa baraza la vijana na jinsi vijana walivyoshirikishwa katika kutoa maoni ya mchakato mzima iliyoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA na kufanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam leo
Baadhi ya vijana wakichangia mada zilizokuwa zikihusu wajibu na haki kwa vijana
Baadhi ya vijana waliofika katika kongamano la kujadili haki na wajibu wa vijana katika jamii.
Victoria Charles ambaye alikuwa ni Mwongozaji wa Mjadala wa Vijana akizungumza na waandishi wa habari leo katoka kongamano lililofanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam
Zulekha Ibrahim kutoka Taasisi la Vijana la TYVA akizungumza jambo
Katibu Mtendaji wa TYVA Saddam Khalfan Ahmed akifunga kongamano la vijana lililowakutanisha vijana ili kujadili haki na wajibu wa vijana. Alisisitiza vijana watafute maarifa na taarifa za maendeleo. Aligusia pia umuhimu wa ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika sekta mbalimbali za maendeleo na vyombo vya maamuzi.
Picha ya Pamoja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: