02/01/2014 - 03/01/2014
Wajumbe wa Bunge maalumu la katiba wameendelea kujadili rasimu ya kanuni zitakazo waongoza katika mjadala wa kujadili rasimu ya pili ya mabadiliko ya katiba ambapo suala la upigaji wa kura limekuwa mjadala mkali kutoka kwa wajumbe waliopata nafasi ya kuchangia.

Baadhi ya wajumbe ambao ni viongozi wa serikali pamoja na wabunge wa chama cha Mapinduzi (CCM) wametaka upigaji wa kura ufanyike kwa uwazi wakati baadhi ya wajumbe ambao ni wabunge wa vyama vya upinzani pamoja baadhi ya makundi wakitaka suala la upigaji kura lifanyike kwa siri.

Akitoa mchango wake wa kanuni hizo Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Mheshimiwa Steven Wassira amesema wajumbe wote ni jamii moja pamoja na kuwa na utofauti wa mawazo anapendekeza kura itakayopigwa iwe ya uwazi kwakuwa hata mataifa mengine yanapiga hivyo.

Kwa upande wake mjumbe mwingine Philemon Ndesamburo akitoa maoni yake kuhusu upigaji wa kura amesema kura ya siri ni muhimu sana kwani ndio njia itakayosaidia kuondoa tofauti katika mjadala huo hivyo suala la uwazi litumike katika kuhesabu kura zitakazopigwa.
Serikali imeahidi kuangalia uwezekano wa kuwafadhili wanafunzi wapatao 20 kutoka katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanaosoma katika chuo kikuu kishiriki cha Stella Maris kilichopo mkoani Mtwara (STEMUCO) ambao hawana uwezo wa kulipa ada ya masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi wakati akimjibu Mhadhiri wa Chuo hicho Padre Aidan Msafiri ambaye aliwasilisha mada yake ya Tunu na maadili katika rasilimali za gesi, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania siku ya pili ya kongamano la viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.

Katibu Mkuu MASWI amesema kuwa serikali ipo tayari kuhakikisha inawapatia elimu hiyo ili waweze kuhudumia jamii ya wananchi wa Lindi pamoja na Mtwara katika kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Bwana Yona Killagane amesema kuwa zipo faida nyingi za mradi wa gesi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kujenga shule za chekechea, wanafunzi kupata udhamini wa kusomeshwa shule za sekondari, kujenga hospitali, maji safi, ajira na kupata umeme unaotokana na gesi katika maeneo yao.

Kongamano la viongozi wa dini ni mwendelezo wa kongamano lilofanyika mwezi januari mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo kauli mbiu katika makongamano hayo ni“Rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Kulia) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wataalam hao waliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Watatu Kulia mwenye koti jeusi) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Wapili Kulia).
Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Kulia) wakitaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi.
Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (aliyenyanyua mkono) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya tanki la kuhifadhia maji kwa ajili ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa.
Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto wa Uwanja wa Ndege wa Iringa (Nduli) ambao ni wanufaika wa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa , Bw. Ranier Nyimbo (Mwenye Fulana nyeusi) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwenye uwanja huo.
Baadhi ya wanavijiji wa Nduli na Kigonzile kutoka manispaa ya Iringa wakichota maji katika bomba pekee linalopatikana katika mpaka wa vijiji hivyo. Adha hii itaisha mwezi Juni mwaka huu mara baada ya kukamilika kwa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ikiwemo wanavijiji hawa. Picha zote na Saidi Mkabakuli

Na Mwandishi Wetu.

Katika kukamilisha ahadi na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 – 2016), Serikali imejidhatiti kuwafikishia maji safi na salama wakazi wa zaidi ya kaya 5000 za Manispaa ya Iringa kufikia katikati ya mwaka huu wa fedha.

Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayodhaminiwa na serikali na wafadhili.

Bibi Mwanri alisema kuwa katika kutimiza Mpango wa huo wa Maendeleo Serikali inawekea mkazo katika Kuendeleza adhma yake ya utekelezaji wa miradi ya maji iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hasa katika maeneo sugu yenye upungufu wa maji hasa maeneo ya vijijini ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuuendelea kuimarisha usimamizi vyanzo vya maji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William alisema kuwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo wa Miaka Mitano zaidi ya vijiji 10 vya mkoa wa Iringa vitanufaika na miradi hiyo ya maji ambayo inagharimu zaidi ya milioni 600.

Maji ni eneo mojawapo la kipaumbele la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaoratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Maeneo mengine
ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango ni pamoja na: miundombinu ya usafiri, nishati; kilimo; viwanda; maendeleo ya rasilimali watu; na huduma za jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna wilaya hiyo inavyoendelea kuboresha huduma za jamii kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizo katika wilaya hiyo.Kushoto ni diwani wa kata ya Kikole Mwl.Haji Mulike na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Ali Mohamed Mtopa.

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam.

Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa umesema kuwa utahakikisha rasilimali zote zinazopatikana katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na gesi asilia zinatumika kuleta maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa huduma za jamii kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizo katika wilaya hiyo.

Akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, watendaji na baadhi ya Madiwani wanaohudhuria kikao kazi jijini Dar es salaam, Bw. Mapunda amesema kuwa halmashauri hiyo imejipanga kupunguza utegemezi wa fedha toka serikali kuu kwa kupanua wigo wa mapato ya ndani kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Amevitaja vyanzo hivyo kuwa vyanzo hivyo vipya ni pamoja na ushuru wa zao la Ufuta ambalo sasa mapato yake yamefikia milioni 595, mauzo ya viwanja na ushuru wa Gesi asilia inayozalishwa katika kijiji cha Songosongo ambayo sasa inatoa asilimia 0.3 ikiwa ni ushuru wa tozo la huduma.

Akifafanua kuhusu mapato hayo Bw. Mapunda amesema kuwa katika zao la ufuta asilimia 20 ya pato hilo inarudishwa vijijini na halmashauri hiyo na kuongeza kuwa mapato ya ushuru wa huduma unaolipwa kwa halmashauri kutokana na shughuli za gesi za kampuni ya PAN AFRICAN ENERGY katika eneo la Songosongo huchangia 20% kwa ajili ya maendeleo ya eneo hilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.

PICHA NA IKULU
DSC_0259
Mjumbe wa Bodi ya Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (Tanzania Human Rights Defenders Coalition) Dkt. Hellen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha watetezi wa Haki za Binadamu nchini na Jeshi la Polisi jijini Dar leo.

.Asema dunia nzima inajua mvunjifu wa kwanza wa haki za binadamu ni dola
.Polisi pia ni binadamu wanahitaji kutetewa na mitandao ya haki za binadamu nchini
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
MKOSAJI na mvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ni serikali kutokana na mazingira halisi ya utendaji na mfumo mzima wa utawala katika serikali nyingi duniani. Imeelezwa.
Akizungumza kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) kwa wakuu na makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo amesema kwa mfumo wa utawala katika nchi nyingi duniani mkosaji mkuu wa haki za binadamu ni serikali.
“dunia nzima inajua kwamba serikali ndio mkosaji mkuu wa haki za binadamu na maana halisi ya serikali ni dola na mahakama tu kwisha,” amesema Jaji Mihayo
Jaji Mihayo amesema kuwa kwa hali ya kawaida dola ikimkamata mtu au mhalifu lazima mpeleke katika mahakama ili sheria ichukue mkondo wake wa kawaida.
DSC_0316
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdurahman Kaniki, akitoa hotuba yake ya ufunguzi kwa niaba ya IGP Ernest Mangu, kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Dkt Helen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi amesema warsha hiyo inatoa fursa nzuri kwa watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi kuboresha kazi zao za utetezi wa haki za binadamu nchini.
Amesema kwa ujumla haki za binadamu hazipewi bali ni haki ya msingi ambayo mtu anazaliwa nayo ili zinaminywa aidha kupitia mtu kwa mtu au taasisi au mfumo wa utawala.
“Kazi za watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi zinaendama na msingi ni utetezi wa haki za binadamu pamoja na mali zao,” alisisitiza
Naye, Mratibu wa kitaifa wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake ya (The Concept of Protection and Security Management for Human Rights Defenders and Social Organization) amesema kuwa taaluma inaweza kutumika kutetea haki za binadamu katika maeneo mengi hapa duniani.
DSC_0334

DSC_0379
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, umuhimu wa kushirikiana kati ya Jeshi hilo na Asasi za kutetea Haki za Binadamu ili kuleta tija katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Amesema pia kupitia mada hiyo kwamba jamii inadhani kwamba anayepaswa kutetewa ni mwananchi tu lakini pia hata polisi naye ni binadamu anapaswa kuwa na mtetezi pale ambapo haki yake ya msingi inapovunjwa.
“Mpaka sasa Tanzania haina sheria yeyote inayomlinda mtetezi wa haki za binadamu lakini tunaendelea na mchakato na ni matumaini yetu serikali itaridhia kuwa na sheria hiyo hapa nyumbani,” alilisitiza
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki amesema kuwa jeshi la polisi nchini litaendelea kuimarisha mahusiano kati ya jeshi hilo na watetezi wa haki za binadamu nia ni kudumisha amani na utulivu nchini.
DSC_0325
Sehemu ya makamishina na makamanda wa mikoa na maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku moja jijini Dar es Salaam.
“majukumu ya jeshi la polisi na watetezi wa haki za binadamu nchini yanafanana kwa kila hali ni kulinda na kutetea haki za wananchi na mali zao,” amesema Naibu IGP Kaniki
Kamishina Kaniki alilisitiza kwamba ni muhimu wadau wote kuzingatia sheria za nchi, taratibu na kanuni katika kutafuta haki mbalimbali ili kudumisha amani na utulivu nchini.
“nachukua nafasi kuwakaribisha wadau wote wa haki za binadamu na makundi mengine kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda na kutetea haki za binadamu nchini,” alisisitiza
Kamanda wa Polisi Arusha, RPC Liberatus Sabas amesema kwa muda mrefu watu wa utetezi wa haki za binadamu na makundi mengine huwa wanasahau kwamba polisi pia ni binadamu nao wanahitaji utetezi kutoka kwa watetezi hao wa haki za binadamu.
DSC_0375

DSC_0417
Naibu Inspekta General wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki (kushoto), Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oparesheni, Kamishina Paul Chagonja wakifuatilia mbalimbali ilizokuwa ikitolewa na washiriki wa warsha hiyo.
DSC_0291
Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake juu ya Ulinzi na utawala wa haki za binadamu kwa mashirika ya watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na Polisi.
DSC_0355
Pichani juu ni Meza kuu na chini ni Baadhi ya Wakuu na Makamishina wa Jeshi la Polisi nchini wakifurahia jambo wakati wa uwasilishwaji wa mada mbalimbali kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
DSC_0362

DSC_0413
Kamishina wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova akichangia mada katika warsha ya siku moja kuhusu Haki za Binadamu na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
DSC_0397
Kamanda wa Polisi, Arusha Liberatus Sabas akizungumza umuhimu wa kujali pia askari polisi kwa sababu na wao pia ni Binadamu wanahitaji utetezi kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea Haki za Binadamu nchini.
DSC_0390
Kamanda wa Polisi, Lindi, RPC Zeloithe Stephen akitoa nasaha kuhusu miiko na kanuni za Jeshi la Polisi jinsi zinavyotetea na kulinda Haki za Binadamu (Police General Order).
DSC_0438
Picha ya pamoja kati ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini na mgeni rasmi Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini.
DSC_0441
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Malya (kulia) akiteta jambo na Kamishina wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova baada ya kupiga picha ya pamoja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. Nyuma yake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe saidi Meck Sadick.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waombolezaji wengine kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.

PICHA NA IKULU
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIKA kukabiliana na uhaba wa walimu nchini serikali imetangaza kuajiri walimu wapya 36,071 ambapo watapangiwa vituo vya kazi mwezi ujao.

Hatua hiyo ni mikakati ya serikali katika kukabiliana na uhaba wa walimu ambapo sasa watakuwa na upungufu wa walimu 21684 kutoka 57755 iliyokuwepo kabla ya kutanga ajira hizo mpya.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, alisema jana kuwa walimu hao watasambazwa katika shule za msingi na sekondari nchini.

Alisema taratibu zote za ajira kwa walimu hao wapya zimekamilika na kwamba mwezi ujao wote walioajiriwa watakuwa wamepangiwa vituo vyao vya kazi.

Majaliwa alisema majina ya walimu wote walioajiriwa na vituo vyao vya kazi tayari kwa kuanza majukumu na serikali itaendelea kuhakikisha uhaba wa walimu nchini unakuwa historia.

Hata hivyo alisema kati ya walimu hao wapya 36021 watakuwa chini ya TAMISEMI na waliobaki watapelekwa kuwa chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Aliongeza kuwa kati ya walimu hao wa ngazi ya cheti ni 17,928 stashahada 5416 na wale wa ngazi ya shahada ni 12,677.

Alisema mgawanyo wa walimu hao uatazingatia na kutoa kipaumbele kwa maeneo na shule zenye uhaba mkubwa ili kuhakikisha changamoto hiyo inaendelea kutatuliwa.

"Tumepanga walimu kulingana na mahitaji ya shule husika ili kuifanya ikama itoshe. Tumetoa maelekezo kwa maofisa elimu na wakurugenzi nchini kuacha tabia ya kuwajaza walimu wengi katika kituo kimoja. Tutasimamia kikamilifu kuwasambaza walimu hao ili kuhakikisha shule zenye uhaba mkubwa zinapewa kipaumbele," alisema.

Alisema baada ya kukamika kwa taratibu walimu wapya wanatakiwa kuanza kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia aprili mosi mwaka huu.

Alisema idadi hiyo inajumuisha walimu wa masomo ya sayansi wa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na walimu wa elimu maalumu.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kila mwaka zaidi ya walimu 40,000 huitimu nchini kutoka kwenye vyuo mbalimbali.

Mwaka jana serikali ilitoa ajira mpya kwa walimu 26,537 wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu ambapo mwaka juzi walimu 23,907 waliajiriwa.
Usikose kuangalia kipindi cha 'The Mboni Show' kinachoruka leo Alhamis kuanzia saa 3 usiku ndani ya EATV, ambapo mablogger Shamim Mwasha wa 8020fashion blog (wa kwanza kulia), John Bukuku wa Fullshangwe Blog (wa pili), na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog pamoja na mwanadada machachali Mboni Masimba ambaye ni mwendeshaji wa kipindi, watakuwa wanazungumzia masuala mbali mbali ya maendeleo ya blog pamoja na mustakabali mzima wa mitandao ya kijamii.
Waombaji 27 kati ya 28 wamerejesha fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ilikuwa leo Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.

Waliorejesha kwa nafasi ya ujumbe ni Arone Benedict Mpanduka, Elizabeth Rashid Mayemba, Emmanuel Augustino Muga, Hassan Maulid Bumbuli, Ibrahim Mkomwa Bakari, Masau Kuliga Bwire, Mbozi Ernest Katala, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa, Salum Amiri Jaba, Tullo Stephen Chambo na Urick Chacha Maginga.
Mhazini Msaidizi ni Elius John Kambili, Zena Suleiman Chande wakati Mhazini Mkuu ni Shija Richard Shija na Mohamed Salim Mkangara.

Katibu Msaidizi ni Alfred Lucas Mapunda, Grace Aloyce Hoka na Ptarick Raymond Nyembera. Katibu Mkuu ni Amir Ally Mhando pekee.

Waombaji nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Egbert Emmanuel Mkoko, Maulid Baraka Kitenge na Mohamed Omary Masenga. Waliojitosa kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni George John Ishabairu, Juma Abbas Pinto.

Ni Shaffih Kajuna Dauda pekee ambaye hakurejesha fomu. Dauda alichukua fomu ya kuwania uenyekiti.
Tume ya Taifa ya imepokea barua kutoka kwa Mhe. Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuiarifu uwepo wa nafasi ya wazi ya Ubunge katika Jimbo la Chalinze lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Saidi Bwanamdogoaliyefariki dunia tarehe 22.1.2014. Baada ya taarifa hiyo, Tume imepanga ratiba ya uchaguzi mdogo katika jimbo la Chalinze kama ifuatavya;

1. Uteuzi wa Wagombea Ubunge utafanyika tarehe 12-Machi-2014
2. Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 13-Machi-2014 hadi 5-Aprili 2014
3. Siku ya kupiga kura ni jumapili tarehe 6-Aprili-2014

Wagombea wanatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Chalinze siku ya uteuzi si zaidi ya saa 10:00 Alasiri. Tume inawaarifu wananchi wote pamoja na vyama vya siasa kufuata tariba iliyotolewa pamoja na kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia siku ya uteuzi hadi siku ya kupiga kura ili watimize haki yao ya kikatiba ya kuvhagua viongozi wanaowataka.

Tume inawasisitiza wananchi wote katika maeneo husika kujitokeza kukagua  taarifa zao wakati wa kuweka wazi daftari la kudumu la wapiga kura ili kuona kama kuna marekebisho madogo yanahitajika kufanyika kuwawezesha kupiga kura bila malalamiko yoyote. Ikumbukwe kwamba hakutakuwa na uandikishaji mpya wa wapiga kura.

Imetolewa na 
Julius Mallaba
Mkurugenzi wa Uchaguzi
Mkuu wa Chuo cha maendeleo ya maji Dr Shija Kazumba akibadilishana mawazo na washiriki wa warsha ya kimataifa kuhusu maendeleo, Miundo mbinu na Vituo vya Maji katikati ni Dr Anderies Jordaan kutoka afrika kusini kushoto aliye vaa shati jeupe ni Afisa Taaluma kutoka UN yenye ofisi zake nchini Ujerumani Dkt. Mathew Kurian Warsha hiyo ya siku mbili ilifanyika hapa nchini na iliwajumuisha watalamu mbali mbali kutoka vyuo vikuu vya kimataifa
Washiriki wa Warsha pamoja na watalamu kutoka chuo cha Maji Tanzania
Dk.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrfod Slaa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiwele katika mkutano wa kampeni wa uchaguzo mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa juzi.
Mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiwele katika mkutano wa kampeni juzi.
Mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega akisalimiana na mmoja wa wazee wa kijiji cha Kiwele, baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo juzi.
MSANII wa filamu nchini Athumani Lali 'Budege' baada ya kucheza filamu za watu sasa ameamua kuja na filamu zake mwenyewe na kuwawezesha wasanii wenzie kuwa na kipato kizuri baada ya kuamua kufungua kampuni yake binafsi inayokwenda kwa jina la AJM Entatainment ambayo ina husika na maswala ya filamu za kibongo.

Athumani Lali 'Budege' akizungumza na mwandishi wa habari hizi Lali amesema kuwa kwa sasa yupo katika atua za mwisho kwa ajili ya kutoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la Faza Hausi ambayo imeshilikisha wasanii wakongwe ndani yake akiwemo Mohamed Nurdini 'Chekbudi', Esha Buheti, Rashidi Mwishehe 'Kingwendu' Muogo Mchungu.
Katika pita pita katika mtandao wa Instagram nimekutana na post ya msanii Peter Msechu ambayo ameelezea tukio la msichana wake wa kazi kufanya jaribio la kujinyonga. Soma alichokiandika mwenyewe...

Mama Mzazi wa msanii wa nyimbo za kizazi kipya, Judith Wambula a.k.a Lady Jaydee, mama Matha Mbibo akipita mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mwanae, Lucy Mbibo wakati wa kuuwaga katika Kanisa la Wasabato lililopo Kiwalani Dar es Salaam jana.
Waombolezaji wakiwa wakiwa katika msiba wa dada yake Msanii muziki wa kizazi kipya, Lady Jaydee wakiwa nyumbani kwao Kiwalani Dar es Salaam jana. Ambapo mwili wa marehemu ulisafirishwa nyumbani kao Bunda Mara.
Meya wa Jiji la Vallejo lililopo California nchini Marekani, Osby Davis (kulia), akimvisha beji Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi baada ya kuzungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akijitambulisha na ujumbe wake wa watu 15. Meya huyo na ujumbe wake wapo nchini kwa mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete kuja kuona fursa za uwekezaji katika jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo mkoani Pwani. Picha na Jumanne Juma
Pichani ni Kamati ya maandalizi ya shindano la utunzi kutoka taasisi ya Tanzania Gatsby Trust (TGT), kutoka ni Mwenyekiti Ibrahim Seushi (kulia) na Mjumbe wa kamati, Profesa Mugyabuso Mlinzi Mulokozi ambaye alikuwa akionyesha picha ya mwasisi wa utunzi.

Kamati ya usimamizi wa Tunzo ya ushairi ya Ibrahim Hussein, kwa kushirikiana na Tanzania Gatsby Trust (TGT) na Mkuki na Nyota, imezindua shindano jipya la ushahiri.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika ukumbi wa Idara Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Ibrahim Seushi alisema kuwa lengo kuu la shindano hilo linafanyika ili kumuenzi mwakilishi wa Tunzo, Marehemu Gerald Belkin ambaye alikuwa mpiga filamu wa Canada aliyeoshi nchini Tanzania katika miaka 1970. Bwana Belkin aliipenda lugha na fasihi ya Kiswahili na alifanya kazi na mtunzi Ebrahim Hussein kuikuza. Alichangia mfuko akitaka uwe chachu ya kuendeleza Kiswahili, hasa utunzi wa mashairi.

Tanzania Gatsby Trust (TGT) ambalo ni shirika linalosimamia mfumo huu, imewashirikisha wajumbe wa kamati kutoka wachapishaji Mkuki na Nyota pamoja na wananzuoni mbalimbali wa ushairi katika kuendesha shindano hili lililofunguliwa leo Februari 26.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Amini Mwinyimkuu amesema kuwa hayupo tayari kumuoa mwanadada Linah Sanga hata kama mlisema amemuimbia wimbo.

Akizungumza jijini Dar na mdaku wetu msanii huyo alisema kuwa watu wengi wamesema juu ya kumuoa Linnah kutonana na gumzo la wimbo wake mpya wa 'Novemba/Disemba' kuwa ni fumbo la harusi yake ambayo amepanga ifanyike kipindi hicho.

Mdaku wetu alidadavua kuwa Amini aliweka wazi kuwa kila kitu kinaenda kwa mipango ila kwa sasa hayupo tayari kuweka wazi kila kitu maana mengine hubaki kifamilia.

'Mniache jamani nipumue wimbo wangu wa 'Novemba/Disemba' msubirie utoe majibu tu, mnayoyataka nyie wenyewe wala msinyumbishwe na maneno ya watu, alisema Amini.

Mnamo mwezi Januari msanii Amini alitoa wimbo wa 'Novemba/Desimba' na kuwa gumzo mpaka mitaani wengine wakasema amemuimbia Linnah, mara oh! Anataka kuona miezi hiyo aliyoitaja...basi ikawa vurugu mechi midomoni mwa watu.
Katibu tawala wilaya Kongwa, Bw Joseph Kisyeli, akimywesha mtoto uji ulioongezwa virutubishi, katika kampeni za uhamasishaji wa chakula cha mtoto chenye virutubishi,katika kata ya ngomai. Zinazoendeshwa na USAID Tuboreshe Chakula ambazo zinaendelea leo
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kongwa, Bw Joseph Mwita Kisyeli, akihutubia wananchi juu ya umuhimu na faida za chakula kilichoongezwa virutubishi,kwa mtoto miezi 6 - miaka 5,katika kampeni ya lishe ilizofanyika kata ngomai wilaya ya Kongwa leo chini ya udhamini wa na USAID Tuboreshe Chakula
Kikundi maarufu cha ngoma wilaya kongwa kata ya ngomai, kikitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa virutubishi zinazoendeshwa na USAID Tuboreshe Chakula katika kata ya Ngomai wilayani Kongwa.
Katibu tawala wa wilaya ya Kongwa na viongozi wenzake wakipata elimu zaidi kwa kusikikiza wataalamu wa lishe kutoka mradi wa USAID Tuboreshe Chakula katika kampeni za lishe zinazoendelea wilayani humo.