MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 27 mpaka 30 ambaye jina lake halijafahamika mpaka sasa amekutwa akining'inia juu ya mti wa Mwembe uliopo katika pori lililopo nje kidogo ya mji wa Pongwe, Mkoani Tanga akidhaniwa kuwa amejinyonga.

Hali ya sintofahamu iliendelea kutanda katika eneo hilo huku kila alieweza kufika katika eneo hilo la tukio akiwa na mshangao wa kipi kilichomsibu mtu huyo mpaka kufikwa na mauti ya aina hiyo.

Akizungumza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaja jina lake litajwe, ameeleza kuwa walipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa kijana mmoja aliyekuwa akichunga ng'ombe katika pori hilo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hali iliyowapekea kwenda moja kwa moja eneo la tukio kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo, lakini kila aliyefika pale hakuweza kumtambua huku wengine wakisema huenda mtu huyo alikuwa ni mgeni kijijini hapo.

Mpaka kamera ya Kajunason Blog inaondoka eneo la tukio hakuna Polisi waliokuwa wamefika.
Sehemu ya Wananchi wakazi wa Mji wa Pongwe Mkoani Tanga wakiangalia mwili wa mtu huyo uliokuwa ukining'inia juu ya mti.Ambapo mpaka ripota wetu anaondoka eneo la tukio hakukuwa na Mwanausalama yeyote aliefika eneo hilo.
Wakazi wa Mji wa Pongwe wakiuangalia mji huo kwa masikitiko makubwa.
Ni uzuni ulikuwa imetawala eneo hilo.
Kila aliepata taarifa hiyo alienda kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo.

Mmiliki wa Kajunason Blog (mwenye shati ya draft) akielekea eneo la tukio.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: