Rais wa Band ya Mashujaa, Chalz  Baba (kushoto), akitoa burudani mbele ya wanahabari Dar es Salaam leo, kuhusu onesho hilo litakalofanyika katika ukumbi huo.. Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Joseph Emanuel na Ofisa Uhusiano wa Band ya Mashujaa, King Dodo la Buche.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Mwandishi Wetu.

MWANAMUZIKI mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Bileku Mpasi, atafanya onesho maalum katika utambulisho wa nyimbo mbili mpya za bendi ya Mashujaa 

utakaofanyika Desemba 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Ten Lounge zamani Business Park.

Akizungumza Dar es Salaam leo  mratibu wa onesho hilo, King Dodoo la Buche, alisema kuwa Mpasi ambaye alitamba katika tasnia ya muziki wa dansi alipokuwa na gwiji, marehemu, Pepe Kale, atakuja na wasanii wengine ili kutoa burudani ya kiwango cha juu.

Dodoo alitaja nyimbo hizo mbili ambazo zitatambulishwa ni pamoja na Rafiki Sokoni na My Queen.

Aliwataka mashabiki wa muziki wa dansi nchini kujiandaa kushuhudia onyesho hilo linalotarajiwa kuwa la kihistoria hapa nchini.

Rais wa Mashujaa Musica, Chalz Baba, alisema kuwa wamejiandaa kutoa burudani nzuri na kuendeleza heshima yao ya bendi bora kwa mwaka wa pili mfululizo.

" Napenda kuwahakikishia wapenzi wa bendi yetu tutafanya kazi ya ubora wa juu, ni kawaida yetu kufanya kazi nzuri, tuna usongo,"  alisema Chalz.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo meneja biashara wa kampuni hiyo Joseph Emmanuel, alisema wameamua kudhamini utambulisho huo ili kuendeleza muziki wa dansi nchini kufikia hadhi ya kimataifa.

Mashujaa pia itatumbuiza nyimbo zake zilizotamba katika albamu zake za Risasi Kidole na Ushamba Mzigo.

Naye Rais wa Mashujaa Chalz Baba amewataka wapenzi wajiandae kupata burudani ya aina yake katika uzinduzi. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: