Ndugu wa Marehemu  Mathew Sebastian Mgimba Philipo Mgimba (katikati) akiwa amebeba msalaba huku pembeni ndugu mwingine akiwa pamoja na picha ya marehemu wakati wa misa fupi ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam leo Novemba 26, 2014.
Dada wa Marehemu Mathew Sebastian Mgimba, Marian (wa kwanza kushoto) akiwa na ndugu zake wakati wa sala ya mazishi iliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni leo
 Rafiki wa Marehemu akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Mathew Sebastian Mgimba mara baada ya sala fupi ya mazishi kufanyika
 Baba Mzazi wa Marehemu Mathew Sebastian Mgimba, Mzee Mgimba pamoja na Mama wakiwa na shada la maua tayari kwa kuweka juu ya kaburi la Mtoto wao Marehemu Mathew Sebastian Mgimba
 Ndugu wa Marehemu Mathew Sebastian Mgimba wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Marehemu Mathew Sebastian Mgimba
 Dada wa Marehemu Mathew Sebastian Mgimba, Bi Mariam Lukaza akiwa na mumewe Johnson Lukaza wakijiandaa kuweka shada la Maua juu ya Kaburi la Marehemu Mathew Sebastian Mgimba katika mazishi yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
Mama Leoncia Lukaza akijiandaa kuweka Shada la Maua kwa niaba ya familia ya Lukaza katika kaburi la Marehemu Mathew Sebastian Mgimba kwenye mazishi ya marehemu Mathew Sebastiani Mgimba yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
Umati wa Watu waliojitokeza kwaajili ya Kumpumzisha Ndugu yetu Mathew Sebastian Mgimba katika makaburi ya Kinondoni. Picha na Josephat Lukaza - http://www.josephatlukaza.com

Marehemu Mathew Sebastian Mgimba alifariki dunia tarehe 20 Nov 2014 nchini Malaysia, Marehemu ameacha Mke na mtoto mmoja. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amin.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: