Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee akifungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam” na kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi  chini ya kauli mbiu isemayo “ Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
  Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza jambo kuhusu athari, madhara  na  ya matumizi ya takwimu zisizo sahihi.
  Baadhi ya wadau mbalimbali na wataalam wa takwimu waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto)  akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu mchango wa matumizi ya takwimu sahihi katika maendeleo ya taifa lolote wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam. unaongeza ushiriki wao katika maamuzi na kuwajengea uwezo wa kutathminiutendaji wa Serikali katika masuala mbalimbali yakiwemo mapato na matumizi. kutathimini matumizi ya Serikali na kushiriki katika midahalo mbalimbali ya kitaifa.
 Mwakilishi


 Msanii Stara Thomas (kulia) akiwa na waimbaji wenzake akiwasilisha ujumbe wa matumizi ya takwimu sahihi kupitia wimbo maalum wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyowashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi  chini.
 Waziri wa Ferdha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee (wa nne kutoka kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu matumizi ya takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo  nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
---
Na. Aron Msigwa – MAELEZO, Dar es Salaam.

SERIKALI kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa itaendelea kuwapatia wananchi takwimu sahihi zinazohusu sekta mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kushiriki katika ngazi za maamuzi na masuala mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Omar Yussuf  Mzee wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yanaoongozwa na kauli mbiu isemayo Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.

Amesema upatikanaji wa taarifa na  takwimu sahihi kwa wananchi

Amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuhakikisha kuwa takwimu mbalimbali zinapatikana kwa urahisi kupitia mtandao, machapisho na mifumo rahisi ili kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali kuzipata pindi wanapozihitaji.

“ Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu yanaongozwa na kauli Mbiu isemayo Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote ambayo inalenga kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi kwa urahisi na kumwezesha mtumiaji kuzipata bila kizuizi chochote” Amesema.

Amefafanua  kuwa upatikanaji wa takwimu huria unawawezesha wananchi kujua sababu zinazoifanya serikali kutekeleza maamuzi mbalimbali, kuongeza uwajibikaji na kuwawezesha kupima matokeo ya sera za Serikali,

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu yameweka msisitizo katika kuweka miundombinu ya kuwarahisishia wadau kupata takwimu sahihi kwa wakati.

Amesema maadhimisho hayo licha ya kujadili masuala mbalimbali yanajikita katika kuweka msukumo wa kuhakikisha kuwa takwimu sahihi zinawafikia wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo bila vikwazo vyovyote ili kuongeza uwazi wa utendaji wa shughuli za serikali serikali.

Naye mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw.Jacques Morisset akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ameeleza kuwa takwimu sahihi ni ufunguo wa maendeleo kwa nchi yoyote duniani.

Amesema kuwa upatikanaji wa taarifa mbalimbali unawawezesha wananchi kutambua na kupima kiwango cha maendeleo ya nchi yao katika masuala mbalimbali yanayogusa maisha yao ya kila siku yakiwemo ya matumizi ya rasilimali, Elimu, ukuaji wa uchumi, shughuli za kilimo na sekta ya viwanda na Biashara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: