Mawakili kutoka Kampuni ya Kamanija and Company Advocates,  wanao mtetea Dk. Juma Mwaka katika kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya maofisa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanaodaiwa kuifunga Kliniki ya ForePlan Herbal iliyopo Ilala, inayomilikiwa na Dk.Mwaka, wakizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo, mara baada ya kusikiliza kesi hiyo ambapo itatolewa uamuzi Novemba 26 mwaka huu iwapo kama upande wa jamhuri utaunganishwa katika kesi hiyo. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Flora Haule. Kutoka kulia ni Wakili Charles Kamanija, Ngassa Ganja na Revocatus Thadeo.
 Mawakili hao wakibadilishana mawazo kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo imewavuta watu wengi wakiwepo wanahabari kutokana na unyeti wake.
 Wakili wa Serikali, Karim Rashid akizungumza na wanahabari kuhusu kesi hiyo. 


Wananchi mbalimbali wakisubiri kusikiliza kesi hiyo.
Mawakili wakizungumza na wanahabri. Wengine ni ndugu na jamaa na wafanyakazi wa Dk.Juma Mwaka.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: