Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba wakipiga ngoma baada ya Waziri, kuzindua Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akionyesha kadi maalum ‘Premier Card’ aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), baada ya kuzindua Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mpango maalumu utakaowawezesha wateja wake wakubwa kufurahia huduma za ziada wawapo kwenye kazi zao. Mpango huu wenye lengo la kuwazawadia wateja wa Airtel utakuwa na kadi maalumu ya kusafirisha yaani (Priority Pass) itayowawezesha wateja wakubwa wa Airtel kupata huduma ya hadhi ya juu kwenye viwanja vya ndege duaniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 pindi watakapo nunua bidhaa na kupata huduma nchini

Kufatia uzinduzi huo wateja wa Airtel sasa wataweza kuunganishwa na huduma za hadhi ya juu kwenye viwanja vya ndege zaidi ya 700 duniani na hivyo kupata viburudisho, urahisi wa huduma yaani (VIP services) pindi wasafiripo na kuwawezesha kufurahia safari zao

Sambamba na hilo wateja hao pia watapata punguzo la hadi asilimia 30 pale watakapopata huduma au kununua bidhaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo hotel, migahawa, maduka makubwa and sehemu nyingine nyingi.

Akiongea wakati wa uzinduzi Waziri wa Nchini katika ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu alisema” nawapongeza sana Airtel kwa kuzindua mpango huu maalumu na kuwazawadi wateja na watanzania nchini. Nafurahi kuona pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano lakini bado tunashuhudia Airtel inajipanga na kujikita katika kuboresha huduma kwa wateja wake.

Natumaini kadi hizi maalumu tunazozindua leo zitawaweza watanzania kupata mwanya wa kutengeneza mahusiano na kutanua wigo wa marafiki wa kibiashara na mwisho kuweza kuvumbua fulsa mbalimbali za kibiashara duniani.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema “ kupitia huduma hii tunadhirisha lengo letu la kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu. Tunauhakika kadi hii maalumu ya kupata huduma zenye hadhi katika viwanja vya ndege mbalimbali duniani hazitarahisha safari zao tu bali zitawawezesha kufanya mahusiano ya muda mrefu ya kibiashara kwa wale watakaokutana nao wakati wa safari.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: