Msanii wa kufanya vichekesho Emmanuel Mathias almaarufu kama Mc Pilipili ameahidi kumfunika mchekeshaji Anne Kansiime wa Uganda katika tamasha linalotarajia kufanyika Agosti 2, 2014 ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Kajunason Blog, MC Pilipili alisema ameshafanya mazoezi ya kutosha, na amejiandaa kutoa burudani ya kutosha ambayo haijawahi tokea sehemu yeyote.

"Kiukweli nimejipanga vizuri maana nilienda kambi yangu niliyoiweka Zanzibar kwa siku 5 na nimerudi Dar es Salaam bado najinoa kumgaragaza Mkali wa kuchekesha na sanaa za majukwaani Afrika Mashariki mwanadada Kansiime ili akienda huko kwao akaadhie alichokutana nacho.

Tamasha hilo la wasanii hao litasindikizwa na litasindikizwa na Fredi Omondi kutoka Uganda na Pilipili wa Tanzania, huku ikinogeshwa na bendi ya ODAMA, imeandaliwa na kituo cha Radio 5.

Emmanuel Mathias almaarufu kama Mc Pilipili mwenye uso wa uchekeshaji kama kazi yake ilivyo, alizaliwa mtaa wa Airport Dodoma mjini mnamo tarehe 1 mwezi wa 10 mwaka 1985 akiwa ni mtoto wa pili wa Bwana Mathias Matebe na Bi Mariam Matebe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: