1. Kuwa karibu na wazazi wako na familia yako pia.

2. Kuwa makini na kila kitu katika maisha yako.

3. Kuwa na kiu ya kuipenda afya yako,kufanya kazi kwa bidii, kula na kuvaaa vyema.

4. Usijihusishe na mambo yasiyo na faida katika maisha yako.

5. Jali thamani yako machoni mwa watu hata kama unapitia katika nyakati ngumu maishani mwako.

6. Usiuabudu umbea.

7. Kuwa makini na marafiki unaowachagua kuwa nao maishani.

8. Usicheze na muda kwa kuamini kesho ipo.

9. Kuwa halisi wakati wa kupanga plan zako na hakikisha kila mara unazipitia kuona kama uko sahihi.

10. Kuwa mwerevu kwa kuishi vyema na jamii inayokuzunguka.

11. Andaa mipango inayoendana na wakati uliopo.

12. Maliza kazi zako kwa muda muafaka.

13. Usilale kwa kuchelewa ukijitetea kuwa unamalizia kazi, panga muda wako kwa kufanya kila jambo kwa wakati wake.

14. Hakikisha unatatua kwa busara, hekima na uvumilivu mkubwa kila tatizo linalokukabili katika maisha yako.

15. Usiwe mtu wa lawama kila mara kwa wakuzungukao.

16. Jitahidi kuwa mtu wa kuyakubali makosa yako na sio kumrushia mwenzako.

17. Heshimu kila anayekuzunguka pamoja na changamoto zao.

Imeletwa kwenu na Fred Kihwele.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Hii nimeipenda mno...ahsante sana kwa misingi hii muhimu katika maisha nami nitaichukua na kuweka pale kwetu ile wengi wajue.

    ReplyDelete