Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiingia  kwenye ukumbi wa mkutano ambao baadaye yeye na viongozi vijana wenzie watakutana na Rais Barak Obama wa Marekani  atakapozungumza nao  jijini Washington DC.

Hii ni sehemu ya program ya mafunzo kwa viongozi wadogo walioonyesha dira toka nchi zote za Afrika (most promising young African leaders). Program hii imeanzishwa na Rais Obama mwenyewe.

Miongoni mwa watanzania wachache waliopata fursa ya kuhudhuria ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Steven Masele na Mhe. Joshua Nassari. Watakutana pia na Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na Mke wa Rais Obama Bi Michelle Obama Pamoja na maseneta, Magavana, wafanyabiashara wakubwa an watu wengine mashuhuri

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: