Hatimaye mtoto Maryline aliyekuwa ameibiwa Changanyikeni jijini Dar es Salaam, amepatikana akiwa Tandale jini Dar es Salaam. Huyo pembeni mwenye tisheti ya blue ndiyo mwizi mwenyewe alikuwa houseboy wao zamani.

Habari zilizodhibitishwa na kutoka kwa vyanzo aminika, vikaleta na picha zimesema mtoto amepatikana. Kijana huyo bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi ili kueleza yaliyomsibu mpaka kupelekea kumuiba mtoto huyo.

HABARI ZA AWALI; INAVYOSEMEKANA...
Huyo kaka alikuwa mfanyakazi wa baba wa mtoto zamani... akaenda kufanya kazi kwingine ambako kutokana na sababu za kwake mwenyewe akawa na deni la 1.6M ambalo wadai wake alipowaambia kuhusu kutokuwa na uwezo wa kulilipa deni ndiyo wakampa akili hiyo ya kuiba mtoto.

Kwa nini alimuiba? je yupo salama na afya njema? Wazazi wataeleza kisa chote. Habari zaidi zitawajia hivi punde endelea kusoma Kajunason Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: