RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume amesema kuwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ina mambo mengi ya kujifunza kutoka China kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia.
Rais Karume aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mahojiano na Waandishi wa habari kutoka vyombo vya Habari vya China wanaofanya kazi zao katika nchi mbali mbali duniani, mahojiano hayo yaliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Katika maelezo yake Rais Karume alisema kuwa Tanzania ikiwemo Zanzibar ni miongoni mwa nchi zinazoendelea hivyo zina mengi ya kujifunza kutoka China kutokana na nchi hiyo kuwa na maendeleo makubwa.
Alisema kuwa hatua ya maendeleo iliyofikiwa nchini China ni ya kupigiwa mfano na kuigwa na nchi nyenginezo zikiwemo nchi zinazoendelea na kusisitiza kuwa mbali na hatua hiyo nchi hiyo pia imeweza kujenga mahusiano na ushirikiano mwema na nchi mbali mbali za Afrika ikiwemo Tanzania.
Rais Karume alisema kuwa Zanzibar na China zina uhusiano wa kihistoria ambao umezidi kuimarishwa hadi hii leo na kueleza kuwa ujio wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China chini Tanzania Mhe, Hu Jintao mwishoni mwa wiki hii kutasaidia kuimarisha uhusiano na ushirikiano huo uliopo.
Alisema kuwa China imeweza kuisaidia Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo afya, elimu, kilimo,viwanda, michezo, habari na msaada wa lami kwa ajili ya ujenzi wa barabara pamoja na misaada mbali mbali ambayo imeweza kusaidia shughuli za kiuchumi,kijamii na kimaendeleo.
Rais Karume alisema kuwa kwa upande wa afya China imesaidia kuleta madaktari pamoja na vifaa vya hospitali na vya mafunzo pamoja na madawa na kueleza kuwa wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakisifu huduma zinazotolewa na madaktari kutoka China.
‘China ina uhusiano mzuri tena wa kihistoria na Zanzibar hali ambayo imeweza kuimarishwa hadi hii leo na kwa kweli China imeweza kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo hapa nchini”,alisema Rais Karume.
Aidha, Rais Karume alisema kuwa China imeweza kusaidia sekta ya kilimo kwa kiasi kikubwa pamoja na sekta ya michezo kwa kujenga uwanja wa Amani ambao kwa hivi sasa unafanyiwa ukarabati mkubwa kwa msaada wa nchi ya China.
Akieleza kuhusu sekta ya habari alisema kuwa China imeweza ksuaidia ujenzi na Studio na mitambo ya redio ya Sauti na Tanzania Zanzibar (STZ), pamoja na Kituo cha Televisheni cha Zanzibar (TVZ) na kusema kuwa China imekuwa ikitoa msaada mkubwa wa masomo kwa Wazanzibari.
Pamoja na hayo, Rais Karume alisema kuwa Zanzibar hivi sasa imekuwa ikichukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha athari za kiuchumi zilizoikumba dunia hazileti madhara hapa nchini kwa kuimarisha huduma za kimaendeleo zilizomo nchini.
Rais Karume pia aliwaeleza waandishi hao wa habari kuwa Zanzibar inawakaribisha wawekezaji kutoka nchini China pamoja na wafanya biashara kuja Zanzibar kuekeza na kushirikiana na wafanyabiashara waliopo nchini ili kuimarisha sekta ya biashara na kuongeza kuwa Serikali imewawekea mazingira mazuri waekezaji na wafanyabiashara.
“Itakuwa ni jambo zuri iwapo patakuwa na mashirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji ambapo wafanyabiasahara na waekezaji watakuja kufanya shughuli zao hapa Zanzibar na wa hapa nao watakwenda China kufanya shughuli zao”,alisema Dk. Karume.
Nao waandishi hao wakiwemo kutoka vyombo vya habari vya ‘Guangming Daily Media Group’, ‘Economic Daily’ na ‘People’s Daily’ kutoka China walitoa shukurani kwa Rais Karume kwa makaribisho yake pamoja na kusifu hatua za maendeleo zilizofikiwa chini ya uongozi wake sanjari na mahusiano na mashirikiano yaliopo kati ya China na Tanzania ikiwemo Zanzibar.
Habari kwa hisani ya Rajab Mkasaba wa Ikulu ZANZIBAR.

Toa Maoni Yako:
0 comments: