Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu mwanadada Miriam Mhembelo sasa ameanza kutamba na video yake iliyoanza kurushwa katika stesheni za tevevion mbali mbali.

Akizungumza na HABARI NA MATUKIO mwanadada huyo alisema kuwa ameamua kuachilia video yake ya "Nafsi yangu" na imekuwa ikifanya vyema katika chat za video za injili.

“Namshukuru Mungu kwa kuweza kunifanikisha kutengeneza video yangu ambayo naona siyo mbaya na imekuwa ikifanya vyema jambo linalonipa nguvu ya kuendelea mbele,” alisema Miriam.

"Kitu kikubwa ninachomshukuru Mungu ni jinsi anavyoweza kunisaidia kupata nafasi ambapo bado namalizia albamu yangu ninayotarajia kuiingiza sokoni hivi karibuni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: