04/01/2008 - 05/01/2008
*** Aitaka Afrika kuongeza sauti yake kuhusu bei za mafuta na chakula

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete (pichani) amelionya Bara la Afrika kuamka na kuanza kutafuta njia za kukabiliana na tatizo la bei kubwa za chakula na mafuta duniani.

Akizungumza katika sherehe ya makabidhiano ya uongozi wa Kamisheni ya AU kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa , Ethiopia , Rais Kikwete amesema kuwa bei hizo ndiyo changamoto mpya na kubwa zaidi kwa wakati huu ya Afrika na uongozi mpya wa Kamisheni ya AU.

Katika makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Kamisheni iliyomaliza muda wake, Alpha Omar Konare wa Mali amekabidhi madaraka kwa Mwenyekiti mpya, Jean Ping wa Gabon .

Kabla ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kamisheni ya AU, Konare alikuwa Rais wa Mali wakati Ping alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Gabon .

Rais Kikwete ambaye alikuwa Mwenyekiti na msimamizi mkuu wa sherehe hiyo, amewaambia mamia ya watu waliohudhuria sherehe hizo:

“Kamisheni mpya inaingia katika madaraka wakati Afrika inakabiliwa na changamoto mbili kubwa sana na mpya. Changamoto hizo ni bei kubwa vya chakula na bei kubwa ya mafuta.”

Ameongeza: “ Kama changamoto hizo hazikukabiliwa haraka na ipasavyo zitamaliza kabisa chumi nyingi za Afrika, ambazo kwa bahati nzuri zimekua zinakua vizuri katika miaka michache iliyopita.”

Rais amesema kuwa iko hatari kubwa kweli kweli kuwa mafanikio yote ya kiuchumi ambayo yamepatikana katika Afrika yatamezwa na bei hizo kubwa za chakula na mafuta.

“Katika hili, sauti ya Afrika inatakiwa kusikika na uongozi katika jambo hili unatakiwa kuonekana dhahiri,” amesema Kikwete.

Mbali na changamoto hiyo ya bei za chakula na mafuta, Rais Kikwete pia aliorodhesha changamoto nyingine zinazolikabili Bara hili kwa kadri uongozi wa Kamisheni unavyotoka mikononi mwa kundi moja kuingia kwa kundi jingine, kwa amani.

Changamoto nyingine ambazo zitaukabili uongozi huo mpya, kwa mujibu wa Rais Kikwete, ni migogoro katika Darfur , Chad , Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Somalia . “Pia hali za DRC, Burundi na Zimbabwe zinahitaji uangalizi wa karibu wa AU.”

Rais Kikwete pia ameutaka uongozi huyo mpya kuongoza mjadala kuhusu utekelezaji wa Azimio la Accra kuhusu mwelekeo wa baadaye wa AU na mapendekezo ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja ya Afrika na pia kuongoza mjadala kuhusu tathmini ambayo imefanywa kuhusu AU yenyewe.

Hata hivyo, Rais ameongeza: “Pamoja na kwamba changamoto ni kubwa na ni nyingi, lakini sina shaka kwamba taasisi yetu iko katika mikono yenye uwezo na yenye uzoefu ya Jean Ping, Makamu wake Erastus Mweche na makamishna wengine wapya.”

Ameongeza kuwaambia viongozi hao wapya“ Hili linanifanya niwe na imani. Kwa niaba ya Serikali na Watu wa Afrika nawaombeni kusimama kupambana na changamoto hizi. Najua mtaifanya kazi hiyo, kwa ufanisi.”

Rais Kikwete pia ameelezea baadhi ya mafanikio ya AU katika kipindi kifupi tokea kuanzishwa kwake kutoka taasisi ya zamani ya Organisation of African Unity (OAU).

“AU sasa imejijenga kama taasisi ya kikanda inayoaminika na inayotegemewa kwenye uwanja wa kimataifa. Matokeo yake ni kwamba AU imejenga ushirikiano wa nguvu na Umoja wa Ulaya, Japan, China, Korea Kusini, Nchi za Marekani Kusini na hivi majuzi na India. Tunatarajia kuwa uongozi mpya utaimarisha mahusiano hayo na kujenga mpya.”

Rais Kikwete pia amemwagia sifa kemkem Konare kwa uongozi wake wa AU. “Profesa Alpha Omar Konare ni mtu wa mawazo mengi na makubwa. Visheni ya AU ya mwaka 2015, kimsingi, ni matunda ya ubongo wake; matokeo ya bongo yake inayochemka na visheni. Ndani ya moyo wa Afrika, kuna sehemu maalum ya Afrika, na watu wake. Ni Mwafrika kweli kweli kwenye sifa ambazo ni ngumu kuzielezea kwa ufasaha wa kweli kweli.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Profesa Alpha Konare ni mtoto wa kweli kweli wa udongo wa Afrika ambaye ameitumia taasisi yetu vizuri sana na kwa ari, moyo mkubwa wa kujitolea na imani kubwa. Profesa Konare siku hizo amekuwa chanzo cha ari kwetu sote.”
no image
WANANCHI wa Jiji la Mbeya wameigomea Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Mbeya ya kutaka kuongeza viwango vya bei ya Huduma ya Maji kuanzia Julai mosi Mwaka huu.

Wakiongea katika Mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) wa kujadili na kutoa maoni yao juu ya maombi ya Mamlaka hiyo, Wananchi hao wamesema kuongeza bei ya Huduma hiyo ni kuwatwisha mzigo mkubwa Wananchi.

Wamesema hawakubaliani na maombi ya Mamlaka hiyo kupandisha Bei ya huduma ya Maji, kwa vile hivi sasa Wananchi wana mizigo mikubwa, ikiwemo ya bei kubwa za Nishati ya umeme.

Wameitaka Mamlaka hiyo itafute vyanzo vingine vya mapato, badala ya kuwabana Wananchi ambao wengi wana kipato cha chini, pia wameiomba Serikali iweke utaratibu wa kutoa ruzuku kwa Mamlaka hiyo ili kuwapa unafuu Wananchi.

Wananchi hao pia wameishambulia EWURA kuwa ni wababaishaji kutokana na kuitisha mikutano ya kukusanya maoni juu ya mapendekezo ya bei mpya za huduma mbali mbali, lakini wakitoa maoni yao hayafanyiwi kazi, na badala yake bei zinaendelea kupanda.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Mbeya imetoa mapandekezo ya kuongeza viwango vya bei ya huduma ya maji kwa asilimia 28.49, kwa Wateja wake wote, isipokuwa wale wa Vibanda(Vioski) ambao wameomba kuwaongezea asilimia tano.
Two military officers of the Tanzania Peoples Defence Forces (TPDF) are in Accra, Ghana through a U.S. Department of Defense sponsored four-day workshop. Lt Col Emmanuel D. Kadaso and Major John M. Mwaipaya, are participating in the U.S.-sponsored Peacekeeping Operations (PKO) Lessons Learned workshop. The two officers will train using U.S. Army methods on how to disseminate lessons learned from exercises, operations and training events with its units and organization across the Army.
(L) U.S. Embassy official, Senior Chief Mark Shafer, Lt Col Kadaso, U.S. Embassy official, Lt Col Patrick Nyaborogo (Retired) and Major Mwaipaya at the U.S. Embassy, Dar es Salaam.
(Photo courtesy of the American Embassy)
Mauaji ya kikatili ya kuchinjwa kama kuku mtoto pekee kwa wazazi wake, Salome Yohana (3) yameumiza wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam na hata nje ya jiji na vitongoji vyake na wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na kitendo hicho.

Akimsimulia safu hii ya HABARI NA MATUKIO jinsi Salome alivyotoweka nyumbani na kukutwa amechinjwa, mama mzazi wa mtoto huyo, Upendo Dustan (27) alisema kuwa siku hiyo ya Ijumaa wiki iliyopita majira ya saa 2.00 usiku aliandaa chakula wakala na mwanaye ambaye baadaye alikwenda kucheza nje na mtoto wa jirani yao.
(Mtoto Ramadhani, siku alipokutwa na kichwa, akiimpa onyo mwandishi kuwa naye hana muda mrefu wa kuishi)
“Wakati mwanangu anaendelea kucheza nje niliamua kuweka neti kitandani ili aje alale na kabla sijamaliza kutandika akaja baba yake akaniuliza alipo mtoto nilimfahamisha kuwa anacheza nje ambapo alikwenda kumuangalia, baada ya muda alirudi ndani akaniambia hajamuona.
“Hata hivyo, shangazi yangu aitwae Furaha Majani ambaye tulikua naye ndani alitoka nje kumtafuta bila mafanikio hali hiyo ilinipa wasiwasi na kunifanya nitoke nje kumuangalia lakini nami sikumuona.
“Baadaye tuliamua kumtafuta kwa majirani lakini hatukumuona, ilibidi tutoe taarifa katika msikiti wa hapa karibu ambapo majira ya saa 3.45 usiku viongozi walitangaza lakini hatukumpata.
“Nilianza kupotelewa na nguvu, hata hivyo, nikiwa na wenzangu tuliendelea kumtafuta hadi saa nane usiku hatukumpata, ilitubidi tupumzike kesho yake asubuhi tulijipanga kumtafuta ambapo wengine walienda vituo mbalimbali vya polisi na baadhi wakaenda kumtafuta hospitalini ikiwemo ya Muhimbili lakini hawakumuona.
(Jirani na aliposimama jamaa ndipo mtoto alipochinjiwa)
Watu walianza kusambaa, lakini katika kundi letu akajitokeza mtoto mmoja akatuuliza kama tumeshampata Salome, nikamueleza bado, alitueleza kuwa kuna kiwiliwili cha mtoto kimeokotwa, alitueleza kilipo na nguo alizovaa, tuliamini ndiye yeye, nguvu ziliniishia nikajitahidi kufika eneo la tukio, nilikuta ni yeye nwanangu Salome (machozi).
“Ilibidi nipige simu polisi ambao walipofika eneo la tukio, walikisaka kichwa cha mwanangu hadi ndani ya choo bila mafanikio na baada ya muda mfupi tulipigiwa simu kuwa kuna kijana mmoja kakamatwa Muhimbili na kichwa cha mtoto, tulikwenda kukiona tulitambua kuwa ni cha mwanangu.

WAGENI WA SEGEREA “Hapa Segerea tulikuja wiki moja iliyopita kumsalimia shangazi ambapo tulimuacha marehemu, mimi na mume wangu tulirudi nyumbani kwetu na Ijumaa tulifika tena hapa na usiku kabla hatujaondoka kurudi kwetu ndipo Salome akawa ametekwa na watu tusiowajua,” alisema Bi. Upendo.
(Marehemu akiwa na wazazi wake enzi za uhai wake)
Baba wa marehemu, Bw. Mussa alipohojiwa alisema kwa kuwa watuhumiwa wamekamatwa hana la kusema isipokuwa kuiachia serikali ili sheria ichukue mkondo wake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi na jana wananchi mbalimbali jijini Dar es Salaam kuhusu tukio hilo, walisema kuwa haingii akilini mwa binadamu kuona mtoto mdogo kama Salome ambaye hana hatia anatekwa na kuchinjwa.
Mkazi mmoja wa Tabata, Bw. Selemani Ali Mtula alisema kuwa mauaji ya mtoto huyo yanatia shaka na inawezekana kuna kundi kubwa la watu wanaofanya unyama huo.
Bishanga alikumbwa na mkasa huo usiku wa kuamkia Aprili 14, mwaka huu nyumbani kwake Makumbusho, jijini Dar es Salaam baada ya jiko la gesi wanalotumia kumlipukia saa 7. 20 usiku.
Kufuatia mlipuko huo, Bishanga aliungua vibaya sehemu mbali mbali za mwili na kupoteza fahamu, hivyo kukimbizwa katika Hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam akiwa hoi bin taaban.
Mwandishi wetu alifanikiwa kufika katika hospitali hiyo na kumkuta Bishanga akiwa amelazwa katika ghorofa ya 2 wodi namba 2 huku mkewe akiwa pembeni yake akimuuguza.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa tabu, msanii huyo alisema kuwa, siku ya tukio alikuwa amelala na mkewe, Terry Godfrey aliyemuoa hivi karibuni na ilipotimu saa 7.20 usiku, alisikia harufu ya gesi ikiwa imetapakaa chumba kizima.
Kufuatia harufu hiyo, Bishanga alisema kuwa alilazimika kwenda jikoni kulikokuwa na jiko la gesi kuangalia kilichotokea, lakini alipofungua mlango tu, mlipuko mkubwa wa gesi ulitokea na kusababisha aungue mwilini.
“Nikiwa nimelala nilishtuka usingizini baada ya hewa kuwa nzito na nilipoamka nilibaini harufu iliyotanda chumbani ilikuwa ni ya gesi hivyo, nikaamua kwenda jikoni kutazama mtungi wake kama ulikuwa una tatizo lakini nilipofungua nilikaribishwa na mlipuko ulioniunguza mwilini kama unavyoniona,” alisema Bishanga.
Kwa upande wake mke wa msanii huyo, Terry alisema kuwa, alishtuka usingizini baada ya kusikia kelele za mumewe aliyekuwa akiomba msaada baada ya kuungua ambapo baba mwenye nyumba naye alisikia kelele hizo hivyo kuungana pamoja na majirani kisha kumkimbiza msanii huyo hospitali. “Mume wangu kipenzi ameungua sana! Sijui ni mkosi gani huu kwani ndoa yetu bado changa, hatujamaliza hata mwaka nakumbana na majaribu makubwa kama haya,” alisema Terry.
TIGO wadhamini wa ziara ya mwanamuziki nyota wa muziki wa Hip Hop toka nchini Marekani, Curtis Jackson maarufu kama ‘50 Cent’ wameweka wazi kuwa sasa wapo kamili kabisa na wataanza kuuza tiketi za kumuona mwanamuziki huyo kuanzia wiki ijayo.

Meneja Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo , Kelvin Twissa ambao ndio wadhamini wakuu wakishirikiana na kampuni ya prime time promotions wanaomleta mwanamuziki huyo hapa nchini,amesema kuwa watauza tiketi chache kukwepa watu kujazana katika onyesho.

“ Tiketi za onyesho la 50 Cent zitaanza kuuzwa Jumatatu ijayo na tutakuwa na tiketi chache ili kuepuka watu kujazana sana kwenye shoo hiyo, hivyo kwa wale mashabiki wa muziki wanaombwa kuwahi kununua tiketi zao ili kuepuka usumbufu” alisema Twissa.

Tiketi za kushuhudia onyesho hilo la 50 Cent zitauzwa kwa Sh 50,000 kwa wale watakaokaa viti maalum, na 30,000 kwa wale watakaokaa sehemu ya kawaida na kuwahi kununua tiketi zao mapema lakini wale watakaochelewa kununua na kununulia mlangonitiketi zao, siku ya onyesho watalipa Sh 40,000.

Onyesho la 50 Cent pamoja na wenzake wa kundi la G-Unit linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa muziki wa Hip Hop hapa nchini limepangwa Kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Mei 4,2008.

Wakati huohuo jana Tigo iliendesha droo ya kwanza ya promosheni kwa wateja wake kwa lengo la kutoa tiketi 200 za kwanza kati ya tiketi 700 zitakazotolewa na Tigo kwa wateja wake ili kushuhudia onyesho la mwanamuziki 50 Cent.Katika droo ya pili ambayo itafanyika wiki ijayo watapatikana washindi 300 na ya mwishoni 200 ili kutimiza washindi 700, watakaoshuhudia onyesho hilo.

Kushiriki katika promosheni hiyo unatakiwa kutuma neno muziki ama ‘Music’ kwenda namba 15315 nabaada ya hapo uatingizwa kwenye droo ya kupata washindi.

Mwanamuziki 50 Cent anayetoka katika jiji la New York nchini Marekani anatamba albamu za ‘Get Rich or Die Tryin’ na ‘Massacre' ambazo zilimpatia tuzo mbalimbali huko Marekani aikiwa na nyimbo kama ‘In da Club’ , ‘I get money’ , Straightto the bank’ na Amusement Park .
no image
BIG BROTHER AFRICA 3 ON DStv!
April 2008
They made their voices heard and now African fans of M-Net’s blockbuster Big Brother Africa can get set for an all-new season 3!
In one of the biggest announcements that the African television operator will make in 2008, M-Net has begun calling for entries for an unprecedented third season of its reality super-series.
With the highlights, drama and excitement of season 2 still fresh in the minds of DStv audiences across the continent, and driven by its phenomenal success,
M-Net has moved quickly to begin work on BIG BROTHER AFRICA 3.
“Audiences clearly demonstrated their involvement with Big Brother Africa 2 by voting, texting the show’s dedicated channel, and downloading video clips,” says Joseph Hundah: M-Net Director of Operations for sub-Saharan Africa.
“With over 900 000 SMS messages received, over 14 million page impressions registered on the show website and over 4 million video clips viewed online, the incredible demand for Big Brother Africa 2 has motivated M-Net to create a third season.”
His comments are echoed by M-Net Director of Original Productions Carl Fischer who says, “Reality TV has proven its appeal with audiences around the world and in Big Brother Africa, M-Net has found an ultra-popular format that crosses boundaries with ease, that entertains broadly across age and gender groupings, and that audiences have shown an unwavering appetite for.”
Now, with BIG BROTHER AFRICA 3 set to launch on Sunday August 24, just hours after the 2008 Olympic Games ends, DStv audiences are in line to receive an extravaganza of great programming.
After 16 days of world-class sporting action, viewers can tune in for 91 days of BIG BROTHER AFRICA action with the Finale scheduled for Sunday November 23.
As with season 1 and 2, in BIG BROTHER AFRICA 3, housemates from 12 countries (Angola, Botswana, Ghana, Malawi, Namibia, Nigeria, Kenya, South Africa, Uganda, Tanzania, Zambia and Zimbabwe) will live together until, after several rounds of public voting, just one will walk away USD 100 000 richer!
With contestants from season 2 now continentally famous, the search is on for 12 new housemates. Do you want to enter Africa’s biggest TV reality series?
To enter BIG BROTHER AFRICA 3, simply collect entry form from your nearest MultiChoice office or log on to www.mnetafrica.com.
Anyone over the age of 21, who is a citizen of one of the 12 participating countries and in possession of a valid passport, can enter BIG BROTHER AFRICA 3. If you’re fluent in English, fun-loving, vocal, creative, original and articulate, then you should definitely enter.
Remember that all entrants must be tolerant of views and lifestyle choices other than their own and must have the social flexibility to live in close proximity with others.
The deadline for entries is Wednesday April 30, 2008.
Once all entries have been received, a selection team will begin evaluating them and short-listing potential housemates, who’ll then undergo a series of medical and physical tests to check their suitability for show’s tasks and challenges.
The 12 individuals finally chosen as BIG BROTHER AFRICA 3 housemates will have no contact with the outside world and will be watched 24/7 by audiences tuned in to DStv channel 198. All programming for Big Brother including the 24 hour channel (channel 198) will have restricted access through the parental guide functionality on the DStv decoder – so parents will be able control viewing of Big Brother.
In addition to DStv channel 198, M-Net will also screen four 30-minute daily shows (Tuesday to Friday) and a late-night ‘Uncut’ show. Audiences can also look out for 60-minute weekly highlights, nomination and eviction shows.
BIG BROTHER AFRICA 3 will be produced by Endemol for M-Net, and Channel O VJ Kabelo Ngakane will once again host the series, screened live from the Big Brother Africa house in Johannesburg.
As with previous editions of the series, audiences will also be able to see Africa’s most creative musicians and performers take their turn on the Big Brother stage, which provides a unique platform to showcase African talent through its widely watched Sunday eviction shows.
Special guests will also make their appearance in the Big Brother house throughout the series, many to promote relevant social awareness programs as in previous years whilst others will be celebrity visitors. As with Big Brother series around the world, of which there have been over 100 international versions, Big Brother Africa 3 promises more great entertainment for African fans.
For now though, it’s your time to shine with just three simple steps. Get an entry, complete it and submit it. Who knows…you may be the next person to win BIG BROTHER AFRICA!
no image
Nusu fainali ya shangwe za utani wa jadi hiyo inakuja, ili kupata kabila lenye shangwe kuliko lingine, lakini hatuwezi kuingia huko kabla ya kuwakutanisha,wasukuma,wapemba,wanyamwezi, wagogo, wandengereko, wahaya, na nikiwasahau wazaramo pwani mtanielewa kweli??

Hapa ni mpepetano,
Wiki hii wakwere wameibuka washindi kwa kuwachezesha waluguru shilanga mwanzo mwisho na waluguru kukimbilia milimani mwee mjomba waluguru tulawa.

Mwendo ni ule ule hatua moja mbele ya pili inafuata jumatatu twaenda kisiwani Zanzibar, Pemba kwa wapemba na wazaramo waliotukaribisha kwenye jiji lao la Dar es salaam,

Kazi kwenu mi nawajuza nanyi mwapiga kura,hebu chagua ,mzaramo na mpemba nani mwenye mzuka wa shangwe kuliko mwenzie ??

Tuma ujumbe wako kwenda namba15584

Shangwe hizi za utani wa jadi ni kwa hisani kubwa ya safari lager, ladha kamili, sifa thabiti.
no image
The BBC is seeking young business minded Swahili-speakers across Africa to take part in its Faidika na BBC (Prosper with the BBC) competition.
Entrepreneurs aged 16 to 24 have until Friday 16 May to submit their proposals on how they can start a successful business that has a positive impact on their community, using US $5,000. The proposal should be no more than 1,500 words and can be emailed to faidika@bbc.co.uk It can also be posted to the following:
Country AddressBurundi Faidika na BBC 2008, Building Maison de la Bible, Avenue de la Mission, 2eme etage, en face de PAR, Bujumbura BP 6790 Kenya Faidika na BBC 2008, 5th Floor, Longonot Place, Kijabe Street, PO Box 58621, Nairobi Rwanda
& DR Congo Faidika na BBC 2008, P.O Box 2790, Kigali Tanzania Faidika na BBC 2008, Skyways Building, 3rd Floor, Ohio Street and Sokoine Drive, Dar es Salaam Uganda Faidika na BBC 2008, 1A, Ruth Towers, Plot 15A, Clement Hill Road, Kampala
BBC Swahili Head, Solomon Mugera, said; “This competition is all about big ideas and giving a young person an opportunity to turn that idea into a viable business. It’s also about helping young people to do well for themselves and serve their local communities.”
Salim Kikeke, Faidika na BBC Project Manager added: “I am convinced many young people have interesting ideas for money-making projects which will launch their business careers. For those who do not win the top prize we hope to offer inspiration and advice to help them get closer to their dreams.”
Five regional heats will take place in Burundi, Kenya, Tanzania, Uganda and Rwanda – which will also include D R Congo finalists. Each regional heat winner will receive a specially commissioned trophy and a certificate. The regional heats takes place in Burundi on Monday, 2 June; Rwanda (with DRC finalists) on Tuesday 3 June; Tanzania on Wednesday 4 June; Kenya on Thursday 5 June; and Uganda on Friday 6 June.
The six winners from the five regional heats will then battle for the top prize at a grand final to take place in Uganda on Wednesday 18 June. The grand final will be broadcast live on BBC Swahili radio and online, via bbcswahili.com. The competition winner will be selected by a panel made up of young East African entrepreneurs and will receive another trophy and US $5,000.
David Ssegawa, aged 22, from Kampala, Uganda, won Faidika na BBC last year. He beat over 5,000 Swahili-speaking new business hopefuls with his award-winning idea - a candle-making business called Bright Light which stops people having to buy imported candles from China. David has now successfully launched his business. To read his story online and find out more about Faidika na BBC go to bbcswahili.com.
We would like to inform you that the Goethe Institute in Dar es Salaam will host a Jazz Concert at the Alliance Francaise on the 25.04.2008 by the group "TRIO IVOIRE-Touching Africa".

It will start at 8 PM and the entrance will be Free.
Sincerely yours,

John Merikion

Division for Development Cooperation,Cultural and Press Affairs
Deutsche Botschaft
•Ubalozi wa Ujerumani German Embassy Umoja House

• Garden Avenue

• P.O. Box 9541Dar Es Salaam / TanzaniaTel: +255 22 2117409
Nani zaidi? Ni swali ambalo sasa Watanzania wanajiuliza kutokana na jitihada kubwa anayofanya Rais Jakaya Kikwete ya kuifanya Tanzania kutambulika kimataifa ikilingashwa na Marais wa nchi nyingine katika Bara la Afrika.


Rais Kikwete mara baada ya kuchaguliwa na Watanzania kuongoza nchi, viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) nao walimchagua kuwa mwenyekiti wa umoja huo, hivyo kuiletea heshima kubwa nchi yetu.
Aidha, ujio wa marais zaidi ya 40 wa Afrika na wake zao na wageni wengine kutoka sehemu mbalimbali za dunia watakaofika nchini Juni 2, mwaka huu katika mkutano wa Taasisi ya Leon Sullivan ni uthibitisho mwingine kuwa uongozi wa Kikwete kimataifa unakubalika.


Kwa mujibu wa Mratibu wa ujio huo wa Marais hao wa Afrika na wageni wengine, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (maelezo) Kassim Mpenda, Tanzania itapokea wageni wanaokadiriwa kufikia 4,000 na lengo kuu likiwa ni kuhimiza wawekezaji kuwekeza nchini hasa katika nyanja ya utalii.
Mpenda alisema hivi karibuni kuwa maandalizi ya ugeni huo mzito kutokea nchini, yanakwenda vizuri na kwamba timu nyingine inayoandaa mapokezi ipo mjini Arusha kwa kuwa nako wageni hao watatembelea.


Alitaja faida kubwa ya ugeni huo kuwa ni katika kujenga nyanja ya utalii kimataifa kwani mara wageni hao watakapoingia nchini, nchi yetu itatangazwa duniani kote na kutoa hamasa kwa watalii kuweza kututembelea.
“Kuja kwa wageni hao yaani marais pamoja na maofisa wengine ni faida kubwa sana kwetu kitalii na kiuchumi kwa sababu watafikia katika hoteli zetu na kulipa pesa, na Rais anajiandaa kuupokea” alisema Mpenda.


Aliongeza kuwa, kamati yake inajiandaa kuanza kutangaza ujio huo ili wananchi waelewe na kuwa tayari kuwapokea wageni hao wazito wa nchi yetu.


Mdau wa utalii nchini, Dk. Ngali Maita alisema Rais Kikwete ameonekana wazi kwamba nyota yake inang’aa kimataifa kutokana na majukumu mbalimbali anayoyapata kimataifa.


Akizungumza kwa simu juzi, Dk. Ngali alisema: “Hakuna haja ya kuogopa kusema ukweli, Rais Kikwete kwa kipindi kifupi sana ameliweka taifa juu kimataifa, leo hii ukiwauliza viongozi mbalimbali duniani kuhusu Tanzania, watakuwa wanaijua, ni kazi nzuri ya JK,” alifafanua mtaalamu huyo wa uchumi alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu ugeni huo unaotarajiwa kuwasili nchini.


Hivi karibuni Rais Kikwete alifanikisha ujio wa Rais wa taifa lenye nguvu za kiuchumi duniani, George Walker Bush wa Marekani ambaye alitoa misaada mbalimbali hasa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.


Ujumbe huo wa Rais Bush, uliweza kutembelea Jiji la Arusha na kuona vivutio mbalimbali vya kitalii ukiwemo Mlima Kilimanjaro.


Aidha, Rais Kikwete pia ameonekana ni zaidi baada ya kufanikiwa kutatua mzozo wa kisiasa ulioibuka nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu kati ya Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Mteule, Raila Odinga.Katika mzozo huo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Kenya, Bw. Samweli Kivuitu alisema alilazimishwa kumtangaza Kibaki hali iliyosababisha ghasia na kuripotiwa kuwa watu wasio na hatia zaidi ya 1,000 walipoteza maisha na mali za mamilioni ya shilingi kuteketezwa moto.


Rais Kikwete pia aliwezesha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kuungana na Majeshi ya Umoja wa Afrika kwenda Comoro kumng’oa Kanali Mohamed Bacar ambaye alijitangazia Urais wa kisiwa kidogo cha Anjoun, visiwani humo.


Hivi sasa JK anatakiwa kwa udi na uvumba nchini Zimbabwe ambako kuna mgogoro mkubwa wa kisiasa kati ya Rais Robert Mugabe na Tsvangirai anayedai kushinda uchaguzi mkuu wa Urais. Mshindi wa urais wa uchaguzi huo hadi jana alikuwa bado kutangazwa.
no image
Kigogo mmoja ambaye katika awamu hii ya nne ya uongozi wa nchi yetu ameukwaa wadhifa wa ukuu wa mkoa na kupangiwa moja ya mikoa ya pwani, amedaiwa kumpachika mimba mwanahabari mmoja mkoani kwake na kusamabaratisha ndoa ya mwandishi huyo.

Habari zinaeleza kuwa kabla ya kigogo huyo kumtundika mimba mwandishi huyo aliyekuwa ameolewa na mfanyakazi mmoja wa benki moja na wakabahatika kuzaa naye mtoto mmoja (majina yao tunayahifahi), alinogewa na penzi la mwanadada huyo jambo ambalo lilimhuzunisha mumewe na kuamua kutengana naye.

Baada kusambaratika kwa ndoa ya mwandishi huyo, imedaiwa kuwa kigogo huyo hivi sasa anaendeleza mapenzi yasiyo na kificho na paparazi huyo.
Imeelezwa kuwa, mara kwa mara dada huyo amekuwa akijivinjari nyumbani kwa kigogo huyo na kutumia gari analolitaka la bosi huyo, isitoshe anapewa heshima zote kama mke na askari wanaolinda usalama nyumbani kwake.

Mpashaji habari wetu amedai kuwa kigogo huyo baada ya kukolezwa na penzi la mwandishi huyo, tayari amemnunulia gari aina ya RAV 4 na kumuwezesha fedha za kujenga nyumba ya familia huku akifanya kila jitihada kulinda habari hiyo isifike kwa wake zake wawili ambao wanaishi nje ya mkoa huo.

Wakati kigogo huyo akitumbua maraha na mwandishi huyo, habari zinasema, wakeze wanaishi kwa dhiki kwani hivi karibuni mmoja wa wanahabari aliyetumwa na mkuu huyo kwenda mkoani kwake kuandika habari za maendeleo alisafiri na mke mmoja wa kigogo huyo kutoka wilayani kwake hadi Dar es Salaam na kuwalazimu kupanda daladala kwenda alipofikia.

Mkuu wa Mkoa huyo ambaye anatajwa kuwa ni kiwembe, awali aliwahi kuripotiwa na vyombo vya habari kuzama kwenye penzi zito la mwanahabari mwingine wa jijini Dar es Salaam ambaye alitaka kufunganaye ndoa lakini muda mfupi baadaye penzi hilo lilisambaratika baada ya mwandishi huyo kupata cheo cha uwakilishi bungeni.

Habari zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa Machi 16, 2008 majira ya saa 2 usiku, mkuu huyo wa mkoa alinaswa na mwandishi wa habari hizi kwenye moja ya hospitali maarufu iliyopo makao makuu ya jiji analofanyia kazi, alimfikisha mwanadada huyo anayeandikia magazeti ya kampuni moja kubwa ya habari nchini ili aweze kujifungua.

Hata hivyo, jitihada za madaktari ziligonga ukuta baada ya kumfanyia upasuaji ambapo mtoto aliyetarajiwa alifariki dunia jambo ambalo linadaiwa kumhuzunisha kigogo huyo.

Habari zaidi zilizopatikana zinasema wanahabari wa mkoa huo, wamekuwa na neema kubwa tangu kuwasili kwa mkuu huyo mkoani humo na sasa humwita shemeji yao.

Alipopigiwa simu wiki iliyopita na mwandishi wetu na kuulizwa kuhusu habari hiyo alikana na kusema kuwa si za kweli. “Habari hizo si za kweli kabisa lakini kama mnajiamini mnaweza kuziandika,” alisema kigogo huyo wa mkoa.
Rais wa china Hu Jintao(kulia) akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa Asia uliomalizika nchini China.

Rais Jakaya Kikwete akimtabulisha Rais wa China Hu Jintao kwa ujumbe kutoka Tanzania aliofwatana nao kwenye mkutano huo nchini China.
Mwanamuziki mashuhuri nchini Tanzania Lady Jaydee, akiwa katika pozi na Mwenge wa Olympic muda mfupi kabla ya mbio za Mwenge huo kuanza jana jijini Dar es Salaam akiwa kama mwanamuziki pekee kutoka nchini aliyeteuliwa kushiriki kukimbiza Mwenge huo.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wa kwanza kushoto akiwa na baadhi ya wabunge wanawake wakicheza mziki(mduara) katika chakula cha jioni alichowaandalia wabunge hao kwenye makazi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.Wapili kushoto ni Naibu Spika Anna Makinda ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Kusini,Kulia ni Mbunge wa Kuteuliwa Bi Zakia Meghji na wa pili kulia ni mbunge wa viti maalum, Bi Anna Abdallah na watatu kushoto ni mgeni kutoka Jamaica , Ingrid Loiten.

Kenya's President Mwai Kibaki (R) meets with opposition leader for Orange Democratic Movement Raila Odinga (L) and his vice president Kalonzo Musyoka (C) after the announcement of his cabinet at state House in Nairobi April 13, 2008. Kibaki named a power-sharing cabinet on Sunday, ending weeks of impasse that threatend to undermine the country's economic recovery after a deadly post-election crisis.


Usafiri wa Dar es Salaam bado ni tabu maana watu hawa bado wanasubiri dala dala; ni vyema tukaweza kuunga mkono makampuni yaliyoanza kutoa matangazo kwa njia ya tiketi jambo litakalofanya kusomwa na watu wengi tofauti na magazeti ambayo wengi wao hawana kipato cha kuweza kununua.


Jambo hili linafanya kampuni ya Tiketi Media kuweza kupata umaarufu kwa kufanya matangazo kwa njia ya kugawa tiketi kama unavyoona huyu mwanafuzi ambaye alikutwa akiwa ameshikiria tiketi yake.
Katika ugawaji wa tiketi haijalishi umri jambo moja ni ujumbe unawafikia vipi walengwa?



BBC inatafuta vijana wenye mawazo ya kibiashara kushiriki katika shindano lijulikanalo kama Faidika na BBC, litakalozinduliwa rasmi Jumatatu Aprili 21 2008.

Faidika na BBC inaalika vijana wanaozungumza Kiswahili, na wenye umri wa kati ya miaka 16 hadi 24, kuwasilisha michanganuo yao, ya jinsi ya kuanzisha biashara ambayo itanufaisha jamii. Mchanganuo huo utatakiwa kuwiana na bajeti ya Dola za Marekani 5,000, zitakazotolewa, ikiwa ni zawadi ya kwanza na kuwa msingi wa biashara hiyo. Mchanganuo usizidi maneno 1,500.
Michanganuo itumwe kwa: faidika na BBC, PPF Building, 8th Floor, P.O Box 79545, Dar es Salaam. Au kwa barua pepe: faidika@bbc.co.uk.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Solomon Mugera, amesema "Shindano hili ni fursa kwa vijana wenye kuona mbali, na ni nafasi yao ya kutimiza ndoto zao. Hii pia ni nafasi kwa vijana kujisaidia wao wenyewe na jamii zao kwa ujumla".
Salim Kikeke, Meneja Mradi wa Faidika na BBC ameongeza "Nina imani kuwa vijana wengi wana mawazo mazuri na ya kuvutia ya kibiashara.
Kwa wale ambao hawatashinda zawadi ya kwanza, tutajitahidi kuwatafutia ushauri wa kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao".
Kutakuwa na mchuano wa kutafuta mshindi mmoja kutoka kila nchi. Kuna jumla ya nchi sita zinazoshiriki katika shindano hili.
Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Mchuano wa kutafuta mshindi wa Rwanda na DRC utafanyika kwa siku moja. Mchuano wa Tanzania utafanyika Jumatano tarehe 4 mwezi Juni. Mshindi kutoka nchi husika atazawadiwa cheti maalum na kombe.
Washindi sita, mmoja kutoka kila nchi zilizoshiriki, watapambana kuwania nafasi ya kwanza mjini Kampala, Uganda, Jumatano, tarehe 18 Juni. Fainali hiyo itatangazwa moja kwa moja kupitia matangazo ya jioni ya BBC, Dira ya Dunia, na vilevile katika mtandao kupitia bbcswahili.com.
Mshindi atapata dola elfu tano za Marekani, pamoja na Kombe. Jopo la majaji litaundwa na wafanyabiashara vijana kutoka Afrika Mashariki na Kati.
David Ssegawa, kijana mwenye umri wa miaka 22, raia wa Uganda, alikuwa mshindi wa Faidika na BBC mwaka jana baada ya kuwashinda washiriki wengine zaidi ya 5,000, kutoka eneo la Afrika Mashariki na kati, wanaozungumza Kiswahili. David aliandika mchanganuo wa utengenezaji mishumaa.
Hivi sasa amekwisha anza biashara yake na inaendelea vizuri. Kupata habari zaidi kuhusu David Ssegawa, pamoja na shidano la Faidika na BBC ingia katika mtandao wetu bbcswahili.com.

Mfanyabiashara mmoja wa madini nchini, ameapa kumpata kimapenzi kisha kufunga ndoa na aliyekuwa mshiriki wa Jumba la Big Brother Africa II (BBA II 2007), Tatiana Durao wa Angola.

Kibopa huyo anayemiliki mashimo kadhaa katika mgodi wa Tanzanite, Mererani mkoani Manyara na mwenye jina kubwa katika orodha ya wafanyabiashara wakubwa nchini, amekusudia kutimiza dhamira hiyo mara baada ya mrembo huyo kuwasili nchini hivi karibuni.

Tatiana, atawasili Dar es Salaam tarehe 22, mwezi huu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo maonesho ya mavazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Muungano pamoja na ufunguzi wa Hoteli mpya ya Naura Springs iliyopo Arusha.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mfanyabiashara huyo (jina tunalo) ambaye anaishi Mbezi Beach, Dar es Salaam, amekuwa akiwatambia washirika wenzake wa kibiashara kuwa ni lazima ampate Tatiana hata kama itamlazimu kutumia robo ya utajiri wake kwakuwa huyo ndiye mwanamke wa ndoto zake.“Dah! Mshirika siku hizi hatulii, tangu aliposikia Tatiana anakuja hapa Bongo, imekuwa tabu kweli kweli.
Kila anachoongea ni kuhusu Tatiana, anasema atahakikisha akifika hapa ni lazima amchukue na baada ya hapo ni ndoa,” kilisema chanzo chetu.Kiliendelea kusema: “Anamsifu Tatiana kwa ucheshi wake, umbo lake na hata sauti yake ambayo mwenyewe anasema inamvutia sana.
Anadai amevutiwa zaidi na sura pamoja na rangi ya mrembo huyo ambayo ina mchanganyiko wa Muafrika na Mzungu.”Kiliongeza kuwa hivi sasa mfanyabiashara huyo amejibatiza jina la utani na anajiita Papa Nyenyere, akimaanisha kuwa atampata Tatiana kwa staili ya kutambaa chini kwa chini kama afanyavyo mdudu nyenyere.
Tatiana aling’ara mwaka jana katika fainali za BBA II na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu. Akiwa katika jumba hilo, Muangola huyo alianzisha uhusiano wa kimapenzi na Richard Bezuidenhout wa Tanzania.



Jana ilikuwa ni siku ya Wanaume Duniani ambapo ulifanyika ule mpambano mkubwa pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.


Katika mpambano huo cha kushangaza kila uliyekuwa unamuuliza vp kuhuduu mpambano wa leo (jana) alionyesha vidole kuashiria kuwa kali ipo.

Mpambano huo ambao ulienda kwa dakika tisini na mshindi kuonekana kushinda bao 5-0 na siyo tena 3-0.
Raundi ya kwanza ilikuwa ya vifijo na vigele gele huku mashambulizi yakielemea upande wa pili yaani wenyewe wanaita 'Side B' kwa Wanaume TMK.

Mpira ulikwenda huku ukiangalia ball postion kuonyesha kuwa ni 75% Wanaume Halisi huku Wanaume TMK kuwa na 25%.


Picha zaidi angalia michuzijr.blogspot.com
no image
Moto mkubwa unaodaiwa kuwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme umesababaisha hasara ya mamilioni ya pesa baada ya kuteketeza sehemu kubwa ya hoteli ya kitalii ya Protea iliyopo katika eneo la Oysterbay Jijini. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jamal Rwambow, amesema tukio hilo limetokea mishale ya saa 7:00, usiku wa kuamkia jana. Amesema moto huo uliteketeza sehemu ya jiko ya hoteli hiyo inayomilikiwa na Rahim Gangiji, 31 na kisha kuteketeza mali yote iliyokuwamo. Amesema moto huo ulizimwa kwa ushirikiano wa wananchi, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Halmashauri ya Jiji na Kampuni binafsi ya Ultimate Security.
Hapa ndio machimbo ya Mererani kama yanavyoonekana, pesa ndiko inakopatikana.
Baada ya migodi ya Mererani kufungwa wachimbaji wa madini (Wanaapolo) maisha yamekuwa magumu na sasa wameanza kutafuta mabaki ya mchanga uliotupwa kutoka kwenye mashimo ili kuangalia kama wataambulia kajiwe cha kuwatoa kwa siku kadhaa.
Makamu wa Rais wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Wanafunzi Kimataifa, Modu Philomena, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho hayo.Kulia ni mlezi wa chama hicho nchini, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi na Makamu wa Rais Masoko na habari, Jokate Mwegelo.
*** TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI***


Pichani ni Mbunge wa kigoma kaskazini (Chadema) Mheshimwa Zitto Kabwe.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda hajasema kuwa Tanzania iko tayari kupeleka jeshi Zimbabwe kama ilivyoandikwa kwa makosa katika gazeti la kila siku la Kiingereza linalochapishwa Dar es Salaam THE CITIZEN toleo la leo (Ijumaa Apr. 11, 2008).
Alichosema Waziri Mkuu katika Bunge mjini Dodoma jana (Alhamisi Apr. 10, 2008) asubuhi wakati wa kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kujibu swali la Mbunge Zitto Kabwe (Chadema) ni kwamba kama ni kupeleka jeshi Zimbabwe basi uamuzi huo utakuwa wa Umoja wa Afrika (AU).
"Kama ni lazima kupeleka jeshi mimi nasema kama ni lazima AU nina hakika itakaa chini itatazama what to do (nini cha kufanya) na kama hapana budi watafanya hivyo," alisema.
Katika swali lake kuhusu hali ya Zimbabwe, Mbunge Kabwe aliuliza kutaka kujua kuwa endapo Jumuiya ya Uchumi ya Kusini mwa Afrika (SADC) iliyotakiwa ikutane kujadili suala la Zimbabwe itaamua kupeleka jeshi la kulinda amani nchini humo kufuatia utata katika matokeo ya uchaguzi, Tanzania itakuwa tayari kupeleka jeshi kama ilivyopeleka Comoro.
Katika gazeti hilo la THE CITIZEN, kwenye habari ya ukurasa wa kwanza, iliandikwa kwa kichwa cha maneno "Dar ready for military action in Zimbabwe", ikimaanisha kuwa Tanzania iko tayari kuchukua hatua za kijeshi Zimbabwe, jambo ambalo kamwe halikuzungumzwa na Waziri na Waziri Mkuu Pinda.
Swali la Mbunge Kabwe na majibu ya Waziri Mkuu, kama yalivyonakiliwa kama yalivyo, katika taarifa rasmi ya Bunge ambayo hupatikana Ofisi ya Bunge ni kama ifuatavyo:-
"MHE. KABWE ZUBERI ZITTO: Mheshimiwa Waziri Mkuu kuhusu Zimbabwe. Mheshimiwa Waziri Mkuu (nchi) yetu imekuwa katika juhudi mbalimbali za kimataifa za kuleta amani, leo tunavyozungumza ni wiki ya pili toka uchaguzi ufanyike Zimbabwe matokeo hayajatangazwa na kuna juhudi dhahiri kabisa Chama cha ZANU-PF ambacho ni marfiki wa chama chako kukataa kukubaliana na matokeo yatakavyokuwa. Serikali ya Tanzania inasemaje kuhusiana na uchaguzi wa Zimbabwe?
WAZIRI MKUU: Haya ningekuwa na uwezo wa kukuuliza na mimi ningesema Kabwe unanishauri nini? Tuseme nini wote (Kicheko/Makofi).
Mheshimiwa Spika, suala la Zimbabwe ni kitendawili si kwa Serikali ya Tanzania lakini ninaweza kusema kwa Afrika yote na ninaweza kusema hata kwa International Community yote, si jambo linalopendeza hata kidogo yaani halipendezi hata kidogo. Na unapokwenda kumsaidia mtu si lazima aonyeshe dalili za kukuomba kwamba Mzee njoo unisaidie kama hujaombwa unaweza ukainuka tu akakwambia nani kakutuma?
Kwa hiyo, unalolisema ni concern (kuhusika) kwa kila mtu sisi wote hapa we are very much concerned (tunahusika sana) lakini aah! mimi nasema ngoja tungoje tuone litakalotokea ni nini.
Tunaye Mwenyekiti wa Nchi za SADC (Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika) kwa hiyo nadhani pengine inaweza ikawa ni kiungo cha karibu zaidi kuliko pengine hata Chairman (Mwenyekiti) wa AU (Umoja wa Afrika). Lakini ni kweli Tanzania sisi tume play role (shiriki) kubwa sana kwa uhuru wa Zimbabwe aah! sasa tungoje tuone litatokea nini maana mimi sina jibu la harakaharaka kwenye eneo hili hata kidogo. (Makofi)
MHE. KABWE ZUBERI ZITTO: Mheshimiwa Spika, mara nyingi tumekuwa tukingoja matokeo yake maafa yanatokea na hiyo huo ni mfano ambao ulitokea Kenya.
Lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu keshokutwa SADC wanakutanaa iwapo SADC wataamua kupeleka jeshi Zimbabwe kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunaweka amani na aliyeshinda uchaguzi anapewa haki yake ya kushinda. Tanzania itakuwa tayari kupeleka Jeshi kama ilivyopeleka Comoro? (Kicheko).
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, bahati nzuri umeliweka vizuri kwamba je kama itaonekana kwamba aliyeshinda uchaguzi na Serikali inaombwa kwenda kuhakikisha huyo aliyeshinda na mifumo mingine inaendelea kazi zake kwa salama bila ya matatizo je Serikali itakuwa tayari kuridhia jambo hili.
Kwa sababu msingi wake mkubwa unanzia hapo lakini so far (mpaka sasa) hatujui nani mshindi lakini tuna taarifa za juu juu tu juu ya jambo hili kwa hiyo mimi nadhani tungoje International Pressure (shinikizo la kimataifa) na mimi najua ipo kubwa, tutakapopata a breakthrough (ufumbuzi) na kwa kweli kama ni lazima kupeleka jeshi nasema kama ni lazima AU nina hakika itakaa chini itatazama what to do (nini cha kufanya) na kama hapana budi watafanya hivyo. (Makofi)"
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM.
Ijumaa Apr. 11, 2008
no image
Jeshi la Polisi Mkoani RUVUMA linamshikilia Mkazi mmoja wa kijiji cha LITOLA katika wilaya ya NAMTUMBO baada ya kukamatwa akiishi kinyumba na mwanafunzi wa darasa la tano.
Kamanda wa Polisi Mkoani RUVUMA Bwana FALHUM MSHANA amesema mtuhumiwa huyo SAID KANDURU mwenye umri wa miaka 38 amekamatwa tangu tarehe 31 mwezi uliopita akiwa amelala nyumbani kwa na binti huyo mwenye umri wa miaka 13.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunafuatia juhudi zilizofanywa na Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha LITOLA Bwana MAXIMILIAN KOMBA aliyeweka mtego na kumnasa usiku wa manane akitumia askari mgambo na wananchi.
Inadaiwa kuwa Mtuhumiwa huyo alikuwa na mawasiliano na bibi wa Binti huyo, kwa makubaliano ya kumwozesha.
Mkoa wa RUVUMA ni kati ya mikoa inayokabiliwa na tatizo la idadi kubwa ya watoto wa shule kukatisha masomo kwa kupata ujauzito, kunakotokana na tabia za baadhi ya wanaume kufanya mapenzi na watoto wa shule.
Kushindwa kwa ushawishi wa kisiasa pamoja na kidini kumetajwa kuwa kunachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vitendo vya rushwa hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi,ofisi ya Makamu wa Rais–Utawala Bora wakati akiungumza na wafanyakazi wa Sekretarieti ya maadiliya viongozi wa umma mjini DODOMA. Mheshimiwa SOPHIA SIMBA (pichani) amesema mmomonyoko wa maadili usiojali walakuogopa maadili ya kazi ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la rushwa hapanchini.
Ameeleza mafanikio dhidi ya rushwa yatategemea kwa kiasi kikubwaushirikiano wa nguvu za dola na kisheria , jamii, dhamira ya kisiasa namaadili binafsi katika kukomesha tatizo hilo haspa nchini.

Mheshimiwa SIMBA amezungumza na wafanyakazi hao wakati wa kufungua mkutano wa sita wa baraza la wafanyakazi na semina ya siku moja kuhusurushwa na huduma kwa wateja inayofanyika mjini DODOMA .

Mapema kamishina wa maadili na mwenyekiti wa baraza hilo lawafanyakazi mheshimniwa Jaji STEPHEN IHEMA amesema kuwa sekretarieti hiyoinatambua kilio kikubwa cha wananchi kuhusiana na rushwa ambapo imewekamikakati ya kupambana na tatizo hilo ndani na nje ya nchi.
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walio katika jeshi la Umoja wa Afrika katika kisiwa cha Anjouani wakishangilia mara baada ya kushiriki katika gwaride la kumpokea rais wa visiwa vya Comoro Ahmed Sambi.
Ni pale mwandishi inapombidi afanye kazi mbili (Pichani ni Mroki Mroki Mwandishi mpigapicha wa gazeti la Habari Leo na Dailynews aliyeambatana na wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walio katika jeshi la Umoja wa Afrika katika kisiwa cha Anjouani , Comoro.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Kalvin Twissa (katikati) akiongea na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Kempinsky, jijini Dar es Salaam juu ya ujio wa mwanamuziki kutoka nchini Marekani 50 Cent ambae anatarajiwa kutua nchi Tanzani mapema mwezi ujao (4th May) na kuwasha moto tarehe hiyo 4th May. Kushoto ni Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Godfrey Kusaga na kulia ni Afisa wa Ongezeko la Thamani wa Tigo, Salim Madati, waandaaji wa ujio huo.
MWANAMUZIKI 50 CENT IMETHIBITISHWA RASMI KUWA WAANDAAJI NI PRIME TIME PROMOTIONS NA WADHAMINI NI WALE WALE WA KAWAIDA - TIGO.
JAMAA ANATUA MAY 4 NA KUTUMBUIZA MEI 4. TIKETI 700 ZITATOLEWA BURE NA WADHAMINI KWA WASHINDI WA MASHINDANO MBALIMBALI YATAYOANZA KARIBUNI.
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE AMANI ABEID KARUME AKISALIMIANA NA BALOZI MDOGO WA CHINA NCHINI BWANA LI,YIPING ALIPOKUTANA NA RAIS IKULU MJINI ZANZIBAR KWA AJILI YA KUJITAMBULISHA.

PICHA KWA HISANI YA IKULU ZANZIBAR.

Kiongozi wa kikuu chama cha upinzani nchini Zimbabwe(MDC) Morgan Tsvangirai
Pichani, anatarajia kutua jijini Dar es salaam muda wowote kuanzia sasa kwa kile kinachoelezwa kuja kuleta malalamiko kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Africa(AU) juu ya hali ya kisiasa nchini zimbambwe baada ya uchaguzi mkuu uliyofanyika nchini humo
hivi karibu ambapo chama cha (MDC) kuibuka na ushindi mkubwa kwa upande wa viti vya wabunge na kusababisha Rais Rober Mugabe kutia ngumu kutoa matokeo ya kiti cha uraisi mpaka sasa.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Imelda Mtema (kushoto) akimkabidhi Bi. Sophia Lupelete (kulia) msaada wa Shilingi 300,000/= (laki tatu) ambazo zimetolewa na wafanya biashara, Amri Premji na Nuresh Vellani ili kumsaidia mama huyo kulea watoto wake watatu wenye ulemavu,katikati ni Afisa utawala wa kampuni hiyo.
no image
Familia ya Bwana Angelo Kajuna wa Kijenge, Arusha wanayofuraha kukualika kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa mtoto wao mpendwa Cathbert itakayofanyika tarehe 10.04.2008, katika kisiwa cha Bongowe kuanzia saa 4usk (22:00hours). Usafiri wa kwenda na kurudi utakuwepo. Pamoja na starehe zote. Kiingilio ni kufika kwako kama utahudhuria toa taarifa usomapo ujumbe huu ili uandikishe jina lako. Asante sana.

***Cathbert Angelo Kajuna ni Mwandishi (Journalist), Mwandishi mpigapicha(Photojournalist), Muandaaji wa vipindi(Programme Producer) na pia ni mmiliki wa blog hii.
Wote watakaopenda kuhudhuria watume ujumbe mfupi(message) kwenye simu no:
+255 713 797 465



Katika shamla shamla za sherehe hiyo nitasindikizwa na rafiki yangu Maru ambaye ameimba wimbo wa Ukweli aliyomshirikisha mwadada Vumilia na pia yatakuwepo makundi mawili ambayo ni maasimu katika muziki wa bongoflava Wanaume TMK na Wanaume Halisi wanaotarajiwa kuchuana April 11 katika mpambano wa Mkali Nani? utakaofanyika ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.

SPEECH OF THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE AT THE OPENING OF THE 5TH MEETING OF THE GLOBAL ALLIANCE TO ELIMINATE LYMPHATIC FILARIASIS

Dr. Mwale Malecela, President of GAELF,

Hon. Ministers from Tanzania, Malawi and Korea;

Members of Executive Group of GAELF,

WHO Representative to Tanzania,


Dr. Mohd Belhocine;


Representative of Merck and Glaxo Smith Klire;


Distinguished Delegates;


Ladies and Gentlemen;


I feel honoured and privileged for the invitation to officiate at the opening of the 5th Meeting of the Global Alliance to Eliminate Lymphatic Filariasis. I would like to thank you for allowing Tanzania to be host to this important meeting. For those many of you who have traveled great distances to attend this conference, I say welcome to Tanzania, the land of Kilimanjaro, Serengeti and Zanzibar.
As Prof. Mwakyusa said, I do hope that at the end of the conference you will find some time to see a bit of our country and experience what Tanzania has to offer in terms of historic and scenic sight as well as flora and fauna. Tanzania has many game parks some of which are only stone throw away from here like the Arusha National Park, the Kilimanjaro National Park with the majestic Mount Kilimanjaro within its borders, Tarangire National Park, Lake Manyara National Park and the Ngorongoro Crater.
For those who would like to venture further, I strongly recommend that you can visit the Serengeti National Park (the 8th new wonder of the world) reknowned for the wilderbeest migration. Fortunately, this time of the year the unique wildlife spectacle is in the Serengeti. You can also go to the spice Island of Zanzibar, the ultimate paradise on the Indian Ocean. I assure you that you will not regret.
Distinguished Delegates, Ladies and Gentlemen;I am very happy to note that this is the first time this meeting is being held in Sub-Saharan Africa. I thank the organization for thinking about Africa and for choosing Tanzania. Africa deserve this kind of treatment. More than one-third of people infected with lymphatic filariasis live in Africa and the social impact of the disease in our continent is immense.
As a person who comes from a country and an area that is endemic with Lymphatic Filariasis, I know how saddening and debilitating the disease can be. Sadly, the physical disabilities caused by the disease are accompanied by social stigma and economic hardship. The cycle of poverty that is perpetuated by this disease is continuous and keeps people trapped with no chance of escape. The disability caused by this disease renders those afflicted unproductive and unable to contribute to national and their individual economic progress.
Here in Africa, lymphatic filariasis exerts a heavy social burden. Often times, this gets especially severe because of the specific attributes of the disease, particularly since chronic complications are often hidden and are considered shameful. As Dr. Mohd Belhocine said, for or men, genital damage is a severe handicap leading to physical limitation and social stigmatization. For women, shame and ridicule are also associated with the disease. People affected by the swelling of limbs are considered undesirables. Marriage which could be a complimentary source of security and pride, is often a difficult matter for the affected.
It is therefore important that we appreciate the efforts being undertaken by the Global Alliance to eliminate this disease from our countries.
The progress that the Global Alliance has made over the past 10 years is phenomenal. I am told that it is the most rapidly expanding programme in the history of Public Health. I understand that the first treatment in Sub-Saharan Africa was in Mafia Island of Tanzania in 2000 and that since then over 1 billion treatments have been given in 44 countries all over the world. This is commendable and I would like to congratulate you all on this mammoth success.
Distinguished Delegates, Ladies and Gentlemen;The past ten years has seen a rapid scale up in the distribution of the requisite drugs to the needy. It has also been a period in which we witnessed the reduction of both infection and disease in several countries. I understand that, at this meeting, Korea will be giving a statement on the elimination of the disease from their country. I have also been made aware that elimination efforts have also been successful in Egypt and, that in Zanzibar, Tanzania, the infection rate has dropped to such low levels that soon Zanzibar will be declared free of lymphatic filariasis.
What this tells us is that it is possible to eliminate this disease to a point where it is no longer a public health problem. This is backed by hard science and empirical evidence through practice. All we need to do is to ensure that these successes are maintained and replicated in other countries.
Ladies and Gentlemen;Whilst there is ample evidence of tremendous success being made, Africa, however, still lags behind in the fight against lymphatic filariasis. Only 11 countries in Africa have active lymphatic filariasis programs. I believe we can do more than that. And, there is no better place to make a bold pronouncement of our resolve to eradicate this disease in Africa than here today. Let us all rededicate our efforts towards that goal.
You may all recall that, in the year 2000 in Abuja, Africa rededicated itself to the fight against Malaria and we have all, without doubt, seen the fruits of this renewed vigour. It is now time to redirect our efforts, with the same vigour, to fight against lymphatic filariasis and other neglected diseases.
Ladies and Gentlemen;I applaud the leadership of Dr. Margaret Chan, the Director General of the World Health Organisation, in raising the profile of tropical neglected diseases and placing a higher priority on them as causes of poverty and hence underdevelopment. We cannot afford perpetuation of diseases that keep our people chained in poverty. Therefore, the fight against these diseases should be considered pivotal to our concerted efforts to fight poverty.
Distinguished Delegates, Ladies and Gentlemen,There are many who say that all Africa needs is economic growth and that all these diseases will disappear. I would say yes and no because they compliment each but more importantly economic growth is greatly hampered by a sick population. My view therefore, is while we pursue economic growth, as governments, we have to deliberately, and in a big way, invest in the health of our people.
I am happy that the global community has come to appreciate that longevity and wellness are key indicators of development. Diseases must be prevented if people are to fully participate in the economic life of their societies. If, we in Africa, are really serious about fighting poverty then the fight against diseases is a battle we must fight and win. This is an integral part of the war against poverty.
Distinguished Delegates, Ladies and Gentleman,The progress since you last met in Fiji has been marked by the recognition of Lymphatic Filariasis as a key part of the neglected disease agenda. The agenda which advocates the use of integrated approaches through Preventive Chemotherapy. Indeed, because of its global distribution, Lymphatic Filariasis is a major platform of this new public health package which is so cheap and cost effective. There are encouraging signs of support from the developed world. As you know, President George Bush of the United States of America announced a new commitment to Neglected Tropical Diseases on his recent trip to Africa to the tune of $350 million over 5 years. This is welcome indeed, we hope to see more of such commitments from the developed nations.
Lymphatic Filariasis is indeed part of this package which is based on the elevation of these diseases higher on the Global Health agenda. We welcome this increased attention to the lymphatic filariasis and other neglected tropical diseases, and how they impact on poverty. These diseases can be eliminated through concerted efforts of African governments, donor nations and agencies as well as the pharmaceutical companies.
Ladies and Gentlemen;I would like to make special recognition of the pharmaceutical companies Merck and Co. and GSK for their generous support in the form free issues of medicines: Avermetin and Albendazole. They are exceptional. They have made it possible for this fight to record the success achieved so far. I am delighted to note that they are continuing to play such a vital role. While we thank so much, these two companies, let me make a humble remind Governments and other responsible authorities in Africa about our responsibility to build on generosity of the donations from the pharmaceutical sector.
Ladies and Gentlemen,I am very impressed that Lymphatic Filariasis patients are a part of the programme for this meeting. It is very important to remember that they are the real reason that we are here. Let us listen to their stories with empathy and humility and keep in mind that our work is not done until this and other neglected diseases are eliminated. Let us work with Lymphatic Filariasis patients, as they can be our greatest advocates in promoting the work that we do in our Lymphatic Filariasis programmes. It is then more than anybody else who demonstrate that your efforts are worth the while.Distinguished Delegates, Ladies and Gentlemen,I would like to end my remarks by renewing my personal commitment and that of my government to the fight against Lymphatic Filariasis. In this regard, I am glad to announce that I have decided to establish the President’s Lymphatic Filariasis Fund to buttress the efforts to fight against this preventable disease. I have committed 50 million Tanzanian shillings to the fund for now to start up. I thank other sponsors for contributing another 17 million shillings making the total start up for the fund a total of 67 million shillings. We would like to raise about 500,000 million in the next few months. Such amount will enable us treat the 15,000 hydrocele patients awaiting surgery.
This fund will directly benefit Lymphatic Filariasis patients in this country and will support hydrocele surgery for those who need it. It will also support those who have lymphoedema and elephantiasis. At the moment, there are 15,000 people registered for hydrocele surgery and that there are many more who are not registered.
I am hoping that these funds will go a long way towards giving support to these and other Lymphatic Filarias patients needing our support. Let me personally thank Tanzania Ports Authority, National Social Security Fund, Tanzania Communication Regulatory Authority, and the New Africa Hotel for their contribution to the fund. I hope others will come forward and contribute to this important cause.
Distinguished Delegates, Ladies and Gentlemen,I know you have a busy schedule ahead of you. Again, I thank you for having invited me here today. And, I wish you all the best in your deliberations. I now have the honour to declare the 5th Meeting of Global Alliance to Eliminate Lymphatic Filariasis open.


God Bless Tanzania.


God Bless Africa.


Thank you for your kind attention

no image
BAADHI ya Watanzania wanaoishi Marekani, wamesema kashfa ya ufisadi iliyoibuka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na Kampuni ya Kuzalisha Umeme wa dharura ya Richmond Development Company LLC, imewadhalilisha.
Katika barua pepe aliyotuma kwa Mwananchi kutoka Jimbo la Carolina kwa niaba ya wenzake, John Mashaka alisema, kutokana na kashifa hizo, wamekuwa wakijiuliza kama wahusika ni wazawa au majambazi kutoka nchi za nje.
Mashaka alisema kutokana na hali hiyo, lazima wahusika wote wakamatwe na isipofanyika hivyo, itakuwa ni kejeli na matusi makubwa kwa walimu, polisi na wafanyakazi wengine wanaofanya kazi katika mazingira magumu.
?Ni jambo la kusikitisha na kutoa machozi, unapowaona watu wachache waliopewa dhamana ya kulinda nchi, wanajaribu kuifilisi na kuchezea jasho la Watanzania wengi, huku watoto wakifa hospitalini kwa kukosa tiba,? alisema Mashaka.
Kuhusu ufisadi, Mashaka alisema unasababishwa na watu kukosa uzalendo na kufanya uamuzi ambao hauna maslahi kwa Watanzania.
?Mtu mwenye ubinadamu katika nafsi yake na mwenye uzalendo na uchungu kwa nchi yake, kamwe hawezi kushiriki vitendo vya aibu kama vile vya Richmond na BoT,? alisema Mashaka.
Akitoa mfano wa Israel, Mashaka alisema nchi hiyo ina uwezo mkubwa kitaaluma kuliko mataifa makubwa yenye uwezo wa uchumi, kutokana na viongozi wake kutanguliza maslahi ya taifa mbele.
Mashaka alisema, Watanazania waishio Marekani, wameridhika na juhudi za Rais Jakaya Kikwete kuboresha maisha ya wananchi na kuweka Tanzania katika ramani nzuri.
Pia, alielezea kuridhishwa na jinsi wabunge wa chama tawala na vyama vya upinzani, walivyoungana na kushirikiana katika sakata la Richmond na kufanikiwa kuwang'oa mafisadi.
Licha ya ufisadi, Mashaka alisema wamefurahishwa na juhudi za serikali kutangaza Tanzania kimataifa hasa vivutio vikubwa vya utalii vilivyopo nchini.
no image
JK afurahishwa Mwenge wa Olimpiki kukimbizwa nchini

Rais Jakaya Kikwete jana (Ijumaa, Aprili 4, 2008) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China katika Tanzania, Bwana Liu Xinsheng. Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu mjini Dar es Salaam.Katika mazungumzo hayo, Mhe Rais na Balozi Xinsheng wamezungumzia uhusiano wa muda mrefu na wa kindugu kati ya nchi hizo mbili.Balozi Xinsheng pia ametumia mazungumzo hayo kumwelezea Mhe Rais kuhusu Mwenge wa Olimpiki ambao utakimbizwa nchini Aprili 13 mwaka huu.Tanzania ni moja ya nchi 20 duniani, na nchi pekee katika Bara la Afrika, ambako mwenge huo utakimbizwa katika mzunguko wake wa dunia kabla ya kurejea Beijing, China tayari kwa Michezo ya Olimpiki inayofanyika nchini humo baadaye mwaka huu.Mhe Rais amefurahishwa na uamuzi wa China kuiteua Tanzania kuwa moja ya nchi ambako Mwenge huo utakimbizwa na kusema kuwa hiyo ni heshima kubwa kwa Tanzania.Wakati huo huo, Mhe Rais pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania katika mji wa Hamburg, Ujerumani, Bwana Jurgein Gothardt.Katika mazungumzo hayo, Bw. Gothardt amemweleza Mhe Rais kuhusu jitihada ambazo anazifanya katika kupata nyenzo za kuweza kutengeneza na kutunza baadhi ya majumba ya kale na ya kihistoria katika mji wa Bagamoyo.Mhe Rais amemshukuru Gothardt kwa jitihada zake na kumhakikishia kuwa Tanzania itafanya kila linalowezekana katika kusaidia juhudi hizo za kulinda na kudumisha historia ya nchi hii.

Menaja Masoko wa Kampuni ya Tiketi Media, Bw. Harold Mwakasala.

Katika ushindani wa kujitangaza kuna makampuni mengi yakiwemo hasa yale ya Magazeti, Television, Radio na Mabango.

Kwa sasa kuna ujio mpya wa kuweza kujitanga ambapo imekuwa rahisi na ujumbe kufika kwa urahisi zaidi na ukijumuisha watu wengi.

Kutokana na hilo Kampuni ya Tiketi Media ndiyo iliyoingia nchini kwa namna yake ya ajabu.

Kampuni hii inayojushughulisha na matangazo kwa njia ya tiketi ambapo mtu inakuwa rahisi sana kupata ujumbe kwa njia hii.

Kampuni hii imeanzishwa mwaka 2006 na kuanza rasmi matangazo mwaka 2008.

Tangazo lake la kwanza lililorushwa na tiketi medii ni la kampuni ya Simu ya mkononi TiGO linalosema shinda safari ya Valentine.

Unaweza kuwasiliana nao kwa simu no 0713 604432

President George W. Bush

President George W. Bush
43rd President of the United States2001 - PresentBorn July 6, 1946

Married to Laura Welch Bush
George W. Bush is the 43rd President of the United States.
He was sworn into office on January 20, 2001, re-elected on November 2, 2004, and sworn in for a second term on January 20, 2005. Prior to his Presidency, President Bush served for 6 years as the 46th Governor of the State of Texas, where he earned a reputation for bipartisanship and as a compassionate conservative who shaped public policy based on the principles of limited government, personal responsibility, strong families, and local control.
President Bush was born on July 6, 1946, in New Haven, Connecticut, and grew up in Midland and Houston, Texas.
He received a bachelor’s degree in history from Yale University in 1968, and then served as an F-102 fighter pilot in the Texas Air National Guard. President Bush received a Master of Business Administration from Harvard Business School in 1975.
Following graduation, he moved back to Midland and began a career in the energy business. After working on his father’s successful 1988 Presidential campaign, President Bush assembled the group of partners who purchased the Texas Rangers baseball franchise in 1989.
On November 8, 1994, President Bush was elected Governor of Texas. He became the first Governor in Texas history to be elected to consecutive 4-year terms when he was re-elected on November 3, 1998.
Since becoming President of the United States in 2001, President Bush has worked with the Congress to create an ownership society and build a future of security, prosperity, and opportunity for all Americans.
He signed into law tax relief that helps workers keep more of their hard-earned money, as well as the most comprehensive education reforms in a generation, the No Child Left Behind Act of 2001. This legislation is ushering in a new era of accountability, flexibility, local control, and more choices for parents, affirming our Nation’s fundamental belief in the promise of every child.
President Bush has also worked to improve healthcare and modernize Medicare, providing the first-ever prescription drug benefit for seniors; increase homeownership, especially among minorities; conserve our environment; and increase military strength, pay, and benefits.
Because President Bush believes the strength of America lies in the hearts and souls of our citizens, he has supported programs that encourage individuals to help their neighbors in need.
On the morning of September 11, 2001, terrorists attacked our Nation. Since then, President Bush has taken unprecedented steps to protect our homeland and create a world free from terror. He is grateful for the service and sacrifice of our brave men and women in uniform and their families.
The President is confident that by helping build free and prosperous societies, our Nation and our friends and allies will succeed in making America more secure and the world more peaceful.
President Bush is married to Laura Welch Bush, a former teacher and librarian, and they have twin daughters, Barbara and Jenna.
The Bush family also includes two dogs, Barney and Miss Beazley, and a cat, Willie.
no image
Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Bw. Philip Parham amesema nchi yake iko tayari kusaidia Tanzania katika harakati za kupambana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

Amesema miongoni mwa maeneo yatakayopewa kipaumbele ni nyanja ya elimu kwa umma ili wananchi waweze kuelewa maana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi na namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

Balozi ameyasema hayo akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Batilda Burian alipomtembelea ofisini kwake jijini leo kwa lengo la kujitambulisha pamoja na kujadiliana naye masuala kadhaa ya mazingira nchini.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Batilda Burian amesema Tanzania kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi hivi sasa Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuzama kwa Visiwa, mfano Kisiwa cha Maziwe huko Tanga, kuyeyuka kwa Barafu katika Mlima Kilimanjaro.

Amebainisha kuwa ili kuhimili mabadiliko hayo ofisi yake imeshaanda Mpango wa Taifa wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi (NAPA) ili kupunguza athari zinazosababishwa na hali hiyo.

Waziri amesema ili kufanikisha programu hiyo ameiomba serikali ya Uingereza kufadhili uchapishaji wa mkakati wa Program ya Taifa ya Kuhimili mabadiliko ya Tabia Nchi ikiwa ni pamoja na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi kupata fursa ya kuisoma na kuelewa.

Dk. Burian amemwomba Balozi huyo kupitia programu yao ya muda mfupi ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi wasaidie katika kujenga uwezo kwa sekta na Wataalamu wanaoshughulika na maafa mfano Mamlaka ya Hali ya Hewa, Idara ya Mazingira, Idara ya Maafa na Vituo vya Tafiti pamoja na kuziwezesha kiteknolojia ili sekta hizo ziweze kukabiliana na matukio mbalimbali yanayotokea.

Aidha, Dk. Burian ameliagiza Baraza la Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na wadau wengine kuunda timu haraka kwa ajili ya kufanya Risk Assessiment katika machimbo ya madini wakianza na eneo la machimbo ya vito vya tanzanite huko Mererani kulikotokea maafa ili waweze kuandaa Mkakati wa muda mrefu wa kufanya Environmental Auditing kwa Maeneo yanayozunguka machimbo hayo. Pia NEMC imetakiwa kuja na mapendekezo ya nini kifanyike katika mkakati wa muda mrefu na kuainisha maeneo yaliyoko kwenye hatari zaidi “Risk Areas”

Balozi Parham katika ziara yake ya utambulisho kwa Waziri aliambatana na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza inayopambana na kupiga vita umaskini duniani Bw. Roy Trivedy.